Mrembo Diana Hussein (kati) amefanikiwa kunyakua taji la Miss Dar Indian Ocean kutoka kwa mwanadada Stella ambaye amemaliza muda wake, mwanadada huyu alifuatiwa na Kudra Lupatu (kulia) na Zulfa Vuai (kushoto). Shindano la Miss Dar Indian Ocean 2012 limefanyika ndani ya Kijiji Cha Makumbusho Dar es Salaam
Washiriki wa Shindano la Miss Dar India Ocean walioingia katika tano Bora wakiwa katika picha ya pamoja.
DJ Choka akiwa na Barnaba na mdau wakifuatilia shindano hilo usiku wa jana kuamkia leo.Kituo hicho cha Miss Dar Indian Ocean kina historia ya kutoa washiriki bomba huku kikiwahi kumtoa Miss Tanzania na Miss World Afrika Nancy Sumary 2005.