Breaking Newzz:Royal bakery ya jkt kawe yavamiwa na majambazi usiku huu,wakomba fedha za mauzo na kuwalaza chini wafanyakazi Mmoja achapwa Makofi

Muonekano wa nje wa Royal bakery mara baada ya Camera ya Jiachie ilipowasili eneo la tukio usiku huu na kukuta difenda ya polisi kutoka kawe ikiwa imewasili eneo hilo,wakati huo huo kukiwa na heka heka za hapa na pale.


Askari wa kituo cha Kawe,wakichukua maelezo kwa baadhi ya wafanyakazi wa bakery hiyo,namna tukio lilivyokuwa,mmoja wa wafanyakazi aliyenaswa vibao akilia kwa uchungu.

Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Royal Bakery hiyo ameeleza kuwa tukio la kuvamiwa na majambazi eneo hilo imetokea mnamo majira ya saa 3 na ushehee hivi (usiku huu),anasema majambazi hao walikuwa watano waliwasili eneo hilo wakiwa na piki piki mbili na gari. Mmoja aliyekuwa ameshika bastola aliingia ndani na kuwaamuru wafanyakazi waliokuwemo ndani wote walale chini,na kuanza kuchukua fedha za mauzo zilizokuwemo kwenye droo zao za kuhifadhia fedha,huku wengine nje wakifyatua risasi hewani na kufunga barabara kwa muda wa dk 10 hivi.


Dada huyo aliyejikuta akiangua kilio wakati akielezea,anasema kuwa yeye amepigwa pigwa makofi na hakujeruhiwa,kama vile haitoshi anasema kuwa eneo hilo pia kulikuwepo na wazungu wapatao watatu ambao walienda pale kujipatia huduma mbalimbali,kwa bahati mbaya wakakutana na dhahma hiyo,ambapo nao walilazwa chini na kuporwa wallet zao sambamba na pete zao walizokuwa wamevaa mikononi,baada ya ambush hiyo majambazi wakatoweka kusikojulikana ndipo difenda ya polisi ikawasili na kuanza kuchukua maelezo kadhaa kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa bakery hiyo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post