Arsenal yasonga mbele kombe la FA

image Thierry Henry amerejea Arsenal kwa kishindo na kuisaidia timu hiyo kusonga mbele katika michuano ya Kombe la FA baada ya kufunga bao pekee katika mchezo dhidi ya Leeds United.

Arsenal wamesonga mbele baada ya kupata ushindi wa bao 1-0.

Henry, 34, alifunga goli lake la 227 kwa Arsenal baada ya kurejea kuichezea klabu hiyo kwa mkopo wa miezi miwili.

Arsenal sasa itakutana na Aston Villa katika raundi ya nne ya kombe la FA katika mchezo utakaochezwa Januari 28.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post