NIJUZE NIJUZE Author
Title: Tanzania yaporomoka viwango Fifa
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
TANZANIA imeshuka kwa nafasi moja kwenye viwango vya ubora wa soka vilivyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa). Tanzania imeshu...

imageTANZANIA imeshuka kwa nafasi moja kwenye viwango vya ubora wa soka vilivyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Tanzania imeshuka kwa nafasi moja kutoka 125 hadi 126 kwa dunia, wakati kwa Afrika ikiwa ya 32.

Lakini kwa Afrika Mashariki Tanzania ipo juu ya Kenya, Burundi na Rwanda, isipokuwa Uganda kwa dunia ipo nafasi ya 82 na Afrika 19.

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Algeria kwenye mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Gabon na Guinea ya Ikweta.

Pia England nayo imeshuka kutoka nafasi ya nne hadi ya nane, licha ya kushinda mechi zake za kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Ulaya, Euro 2012.

Kikosi hicho cha Fabio Capello kiliifunga Bulgaria mabao 3-0 mjini Sofia kabla ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wales.

Bingwa wa Dunia na Ulaya, Hispania, imerudi katika nafasi yake ya kwanza ikifuatiwa na Uholanzi iliyoshuka hadi nafasi ya pili, Ujerumani ya tatu na mabingwa wa soka la Amerika Kusini, Copa America, Uruguay wakishika namba nne.

Ureno imeshika nafasi ya tano, huku Italia ikijivuta hadi nafasi ya sita, Brazil nafasi ya saba, Croatia tisa na Argentina namba 10.

Kwa upande wa Afrika, Ivory Coast imeshika nafasi ya kwanza na 16 duniani ikifuatiwa na Misri huku kimataifa ikishika nafasi ya 36.

Ghana kwa Afrika inashika nafasi ya tatu wakati kwa dunia 37, huku Burkina Faso ikishika nafasi ya 41 kwa dunia, wakati Afrika ni ya nne, Senegal inashika nafsi ya tano Afrika na kwa dunia ni ya 42.

Nigeria imeshika nafasi ya sita Afrika na ya 43 ya dunia, Algeria namba saba Afrika 46 ya dunia, Cameroon nafasi ya nane Afrika 48 ya dunia, Afrika Kusini nafasi ya tisa Afrika 51 ya dunia na Morocco nafasi ya kumi Afrika 59 ya dunia.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top