NIJUZE NIJUZE Author
Title: Man U na Chelsea zakosa kufunga magoli mengi
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Wayne Rooney alifunga bao lake la tisa msimu huu wa ligi kuu ya Premier ya England, na kuiwezesha Manchester United, ikicheza katika uwanja ...

Wayne Rooney alifunga bao lake la tisa msimu huu wa ligi kuu ya Premier ya England, na kuiwezesha Manchester United, ikicheza katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumapili, kuifunga Chelsea magoli 3-1.

imageMchezaji huyo wa timu ya taifa ya England aliweza kufunga bao la tatu, baada ya wenzake Chris Smalling kufunga bao la kichwa kufuatia mpira alioupata kutoka kwa Ashley Young, na Nani alikuwa pia amefunga la pili kutoka yadi 25.

Mara tu baada ya kipenga kuashiria kipindi cha pili kuanza, Fernando Torres aliweza kuandikisha haraka bao lake la pili akiichezea Chelsea na kuwapa mashabiki wengi matumaini ya kusawazisha mambo katika kipindi cha pili.

Chelsea walipata moyo zaidi wa mambo kubadilika, hasa Rooney alipokosa kufunga kupitia mkwaju wa penalti, walioipata Man U baada ya Jose Bosingwa kumwangusha Nani.

Wasiwasi wa pekee kwa Sir Alex Ferguson, meneja wa Man U, ilikuwa ni kumtizama Javier Hernandez akichechemea katika kipindi cha pili, kufuatia Ashley Cole kumfanyia rafu katika mguu wake.

Kulikuwa na matumaini ya Torres kuhakikisha angalau mechi ilikwisha kwa Chelsea kufungwa magoli 3-2, lakini mguu wake ulithibitisha kabisa ulishindwa kutimiza wajibu wakati huu, kwani mpira ulielekea juu, huku lango likiwa wazi kabisa.

Katika mechi nyingine za Jumapili, mpira kweli hauna adabu, na usiwacheke wenzako kwa kufungwa.

Emmanuel Adebayor

Adebayor alifunga magoli mawili katika mechi yake ya kwanza uwanja wa nyumbani wa White Hart Lane.

Liverpool waliaibika kwa kufungwa na Tottenham katika uwanja wa White Hart Lane magoli 4-0.

Msimu huu inaelekea kila timu inataka kuweka kibindoni magoli mengi, kwani Sunderland, katika ushindi wake wa kwanza msimu huu, pia iliizaba Stoke magoli 4-0, kufuatia kutambua wapinzani wao walikuwa dhaifu mno katika kuimarisha ngome yao.

Emmanuel Adebayor, ikiwa ni mechi yake ya kwanza katika uwanja wa nyumbani tangu kusajiliwa na Tottenham, alifunga magoli mawili, na Luka Modric na Jermain Defoe pia wakifunga.

Majirani wa Man U, Man City, walishindwa kuwika katika uwanja wa Craven Cottage, kwani licha ya kuongoza kwa magoli 2-0, hatimaye mchezo ulimalizika kwa sare ya 2-2.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top