Boas asema matokeo na United si muhimu

imageKocha wa Chelsea Andre Villas-Boas amesema matokeo ya mechi kati ya Chelsea na Manchester United siku ya Jumaapili "hayatamaanisha chochote kwani ni mapema sana kuleta athari yoyote kwa mchuano wa ligi."

"Umuhimu wetu katika mchezo huo ni mdogo mno. Ni juu ya wachezaji kutumia umahiri wao na kufurahia mchezo wao. Kocha yeyote atakayehukumiwa baada ya mechi tano tu inamaanisha kasoro haziko kwa kocha bali kwa watu wanaosimamia vilabu."

Kushindwa kwa Chelsea kutaiweka klabu hiyo pointi tano nyuma ya Manchester United, lakini wakishinda wataipiku United kwa pointi moja zaidi.

Mechi hii inawakutanisha mojawapo wa makocha wa muda mrefu, Ferguson dhidi ya mojawapo wa makocha vijana kabisa ,Villas-Boas.

Villa Boas alikua na umri wa miaka 9 wakati Sir Alex Ferguson alipochukua hatamu za kuinoa Manchester United.

Kwa mara nyingine Chelsea haitamchezesha Didier Drogba, ambae alipoteleza fahamu wakati Chelsea ilipoishinda Norwich wiki tatu zilizopita. Kwa hiyo kocha Villas-Boas itampasa aamuwe kama kuanza na Fernando Torres ama Nicolas Anelka.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post