NIJUZE NIJUZE Author
Title: Arsenal yaanza ligi, Man City yaua 3-0
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Sergio Aguero amefunga mabao matatu peke yake wakati Manchester City ilipoonesha kandanda safi dhidi ya Wigan na kuisadia timu hiyo kuendele...

Sergio Aguero amefunga mabao matatu peke yake wakati Manchester City ilipoonesha kandanda safi dhidi ya Wigan na kuisadia timu hiyo kuendelea kupanda kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Soka ya England.

Sergio Aguero

City wakisakata soka ya kuvutia walipata nafasi nyingi za kufunga kabla ya Aguero kuanza kuziona nyavu dakika ya 13 kwa mkwaju aliouchonga pembeni baada ya pasi ya David Silva.

Carlos Tevez alikosa kufunga baada ya mkwaju wake wa penalti kuokolewa, kabla ya Micah Richards na Vincent Kompany mikwaju yao kugonga mwamba.

Lakini baada ya kosakosa hizo Aguero akafunga mabao mawili ya haraka haraka.

Nayo Arsenal ikizawadiwa nafasi ambayo Andrey Arshavin hakufanya makosa na kuipatia bao Arsenal lililoiwezesha timu hiyo kupata ushindi wake wa kwanza katika ligi msimu huu.

Andrei Arshavin

Mpira aliokuwa akiurusha mlinda mlango wa Swansea Michel Vorm ukamgonga mlinzi wake Angel Rangel na ukatua katika miguu ya Arshavin aliyeujaza mpira kimiani.

Arshavin, ambaye hivi karibuni alikuwa akishutumiwa kwa kushuka kiwango, alifunga bao hilo taratibu akiwa katika kona ngumu huku lango likiwa wazi halina mlinda mlango.

Nafasi nzuri ya kusawazisha kwa Swansea ilitokea wakati mkwaju wa free-kick uliopigwa na Scott Sinclair ukagonga nguzo ya juu ya lango la Arsenal na kutoka nje.

Kwa upande wa Chelsea Juan Mata alianza mechi yake ya kwanza tangu mwanzo, iliisaidia timu hiyo ikiilaza Sunderland kwa mabao 2-1, licha ya Sunderland kupata bao dakika za mwisho.

John Terry

John Terry alikuwa wa kwanza kufunga bao baada ya mkwaju wa free-kick uliopigwa na Mata kugonga nguzo na kumkuta Terry aliyemalizia.

Na Daniel Sturridge alimalizia kazi kwa kufunga bao kiufundi kwa kisigino na mpira kumpita mlinda mlango Simon Mignolet na kufanya matokeo yasomeke 2-0.

Ji Dong-Won aliipatia Sunderland bao la kufutia machozi dakika za mwisho za mchezo.

Emmanuel Adebayor amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza akianza kuichezea Tottenham na timu hiyo kuanza kufunga tangu msimu huu uanze dhidi ya Wolves.

Adebayor

Baada ya bao hilo la kwanza timu hizo zilionekana kushambuliana kwa zamu, na mlinda mlango Brad Friedel alifanya kazi kubwa alizuia mkwaju wa Karl Henry na Niko Kranjcar alilazimika kuokoa bao katika mstari wa lango.

Lakini alikuwa Adebayor aliyefanikiwa kufunga bao lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Tottenham baada ya kubanwa kitambo, baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa Scott Parker, akamzunguka mlinda mlango na kuujaza mpira mavuni.

Na Jermain Defoe akahitimisha kazi kwa kufunga bao maridadi kwa mkwaju wa chinichini katika dakika ya 80.

Stoke ilimaliza rekodi ya Liverpool ya kutofungwa msimu huu baada ya Jonathan Walters kufunga kwa mkwaju wa penalti.

Jonathan Walters

Walters aliangushwa wakati akiwania mpira na Jamie Carragher na hakufanya makosa kupachika bao.

Ryan Shawcross alimbana vilivyo Luis Suarez aliyekuwa katika harakati za kuisawazishia Liverpool.

Bao la dakika za mwisho la kusawazisha lililofungwa na Gabriel Agbonlahor liliiwezesha Aston Villa kwenda sare ya mabao 2-2 baada ya Everton kuonekana kuumiliki mchezo.

Gabrile Agbonlahor

Leon Osman ndiye aliyeanza kuipatia bao Everton kwa mkwaju wa yadi 12 kipindi cha kwanza na walionekana wakilalamika wamenyimwa mkwaju wa penalti wakati Barry Bannan alipomfanyia rafu Leighton Baines.

Villa ilisawazisha kwa mkwaju wa Stiliyan Petrov aliyeuachia mita 30, lakini Everton wakafanya matokeo yaonekane 2-1 baada ya Fabian Delph kumfanyia rafu Phil Jagielka.

Mkwaju wa krosi iliyochongwa na Marc Albrighton ilitumiwa ipasavyo na Agbonlahor aliyefunga kwa kichwa na matokeo kumalizika 2-2.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top