NIJUZE NIJUZE Author
Title: Wanawake wanaovuta sigara hatarini kuliko waume
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Utafiti mpya umeonyesha kwamba wanawake walio na uraibu wa kuvuta sigara wako katika hatari ya kupata maradhi ya moyo zaidi kuliko wanaume ...

Bibi mvuta sigara

Utafiti mpya umeonyesha kwamba wanawake walio na uraibu wa kuvuta sigara wako katika hatari ya kupata maradhi ya moyo zaidi kuliko wanaume walio na uraibu huo.

Utafiti ulioendeshwa miongoni mwa zaidi ya watu milioni mbili umepata wanawake wako kwenye hatari ya maradhi ya moyo kwa asili mia 25 wakati wanapotumia tumbaku.

Sababu za matokeo haya hazijatolowa japo watafiti kutoka Marekani wamesema wanawake wako kwenye hatari kubwa ya kuvuta kemikali zenye sumu kutoka kwa sigara ikilinganishwa na wanaume.

Hali hiyo wameongeza imejitokeza katika idadi ya wanawake wanaopata saratani ya mapafu ikilinganishwa na wanaume wanaovuta sigara.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top