NIJUZE NIJUZE Author
Title: MAAJABU YA ULIMWENGU
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Bwana mmoja nchini India aliyekwenda hospitali kutokana na maumivu ya tumbo, alifanyiwa upasuaji na madaktari kukuta bwana huyo ameota kiza...

image

Bwana mmoja nchini India aliyekwenda hospitali kutokana na maumivu ya tumbo, alifanyiwa upasuaji na madaktari kukuta bwana huyo ameota kizazi cha kike.

Bwana huyo, ambaye kazi yake ni mkulima, na tayari ana watoto wawili, alitajwa kwa jina la Ryalu, na gazeti la Telegraph, ambalo limeandika taarifa hii.

Mtandao wa cnews.com umesema madaktari walidhani kuwa bwana huyo anasumbuliwa na ngiri.

Hata hivyo baada ya madaktari kumfanyia upasuaji, walikuta akiwa na viungo kamili vya uzazi vya kike.

Bwana huyo alikuwa akiishi maisha ya kawaida kabisa, huku viungo vyake vya kiume vikifanya kazi kama inavyotakiwa.

"Viungo vyake vya kiume viko sawa kabisa" amesema Daktari Pramod Kumar, akizungumza na gazeti la Telegraph. Bwana huyo ameondolewa viungo visivyo vyake, na anaendelea vizuri hospitali

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top