NIJUZE NIJUZE Author
Title: Mgao wa Umeme kuongezeka zaidi Tanzania
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Tanzania imeongeza mgao wa umeme na kuufanya kuwa mkali zaidi kutokana na vyanzo vyake katika mabwawa ya umeme kupungua maji. Mabwawa hayo y...

imageTanzania imeongeza mgao wa umeme na kuufanya kuwa mkali zaidi kutokana na vyanzo vyake katika mabwawa ya umeme kupungua maji. Mabwawa hayo yamepungua maji kwa kiwango kikubwa kutokana na ukame.

Lakini Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limeahidi maeneo muhimu kama hospitali hayata athiriwa na mgao huo.

Afrika Mashariki inaripotiwa kuathiriwa na ukame mkali kwa miaka 60 iliyopita.

Watu wapatao milioni 10 wanahitaji msaada wa chakula hasa nchini Somalia, Kenya na Ethiopia.

Tanzania inategemea zaidi ya nusu ya vyanzo vyake vya umeme kupitia mabwawa hayo.

Msemaji wa TANESCO Badra Masoud, ameiambia BBC Idhaa ya Kiswahili kuwa upungufu wa mvua ndio chanzo cha matatizo hayo kutokana na mabwawa kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

"Kutakuwa na mgao lakini hautakuwa wa saa 24," alisema.

"Baadhi ya watu hawatakuwa na umeme kati ya saa mbili za usiku mpaka saa sita na wengine wakosa kuanzia saa 12 hadi saa tano usiku ( saa za Afrika Mashariki.

"Lakini maeneo ya Hospitali na kwenye pampu za maji hazitaathiriwa," alisema Bi Masoud.

Mabwawa ndio chanzo kikubwa cha umeme kwa TANESCO huku gesi na mitambo ya umeme vikichangia kiasi kilichobaki.

Mabwawa hayo yanatarajiwa kuanza kujaa tena msimu wa mvua utakapoanza mwezi Septemba.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top