Unknown Unknown Author
Title: HUU NDIO UAMUZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI JUU YA WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUTOKA TANZANIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ni muda mfupi uliopita jopo la majaji wa mahakama ya Afrika mashariki huko Arusha imetoa uamuzi wa Shauri ambalo ilifunguliwa na CHADEMA...
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki
Ni muda mfupi uliopita jopo la majaji wa mahakama ya Afrika mashariki huko Arusha imetoa uamuzi wa Shauri ambalo ilifunguliwa na CHADEMA ( Antony Komu ) aliyekuwa mgombea wa Chadema katika Bunge la Afrika mashariki , ambaye alifungua kesi ya msingi kuhusu kukiukwa kwa hati ya makubaliano ya Afrika ya mashariki , kutokana na Chadema kutokupata nafasi wakati hati iko wazi na imeelezea kinagaubaga jinsi ya kupata wawakilishi kutokana na uwiano wa vyama katika mabunge ya nchi washirika .

Mahakama ya Afrika mashariki, imesema kuwa Bunge na serikali walikiuka hati hiyo ibara ya 50 , na pia kitendo cha kumpa fursa kugombea John Lifa Chipaka wakati chama chake hakina mbunge ni muendelezo wa kukiukwa kwa hati hiyo ya Afrika mashariki .

Jopo la Mawakili wa Chadema lilikuwa likiongozwa na Edson Mbogoro , Aidha mahakama imeitaka serikali kulipa Antony Komu gharama zote za kesi .

Kwa mliofuatilia mtakumbuka kuwa kulikuwa na ubishani mkubwa sana wa kikanuni ndani ya Bunge siku ya uchaguzi huo, hukumu hii itasaidia sasa ile kesi ya pili ambayo iko mahakama kuu Dodoma ya kuitaka mahakama hiyo itengeneze uchaguzi ule na Urudiwe upya kuendelea kwa kasi.


********************************************
LindiYetu.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani, Siasa, Michezo ya Africa na Nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram Twitter Na Facebook

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top