YANGA YAITANDIKA DODOMA JIJI 2-0 | NBC PL

Young Africans imeendeleza ubabe wake katika ligi kuu Tanzania Bara, baada ya kuweka rekodi ya kutofungwa katika michezo 48 Ligi Kuu.

Yanga imeweka rekodi hiyo baada ya ushindi dhidi ya walima zabibu wa Dodoma, Dodoma Jiji wa goli 2-0 katika uwanja wa Liti mjini Singida.

Fiston Mayele ndio aliyeifungia Yanga Magoli hayo mawili, La kwanza ni baada ya kuitumia vizuri krosi ya Tuisila Kisinda katika dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza na Goli la pili alipokea pasi kutoka kwa Denis Nkane na kuweka kambani mnamo dakika ya 67.

Kwa matokeo haya Yanga inarejea kileleni na kumshusha Azam Fc ikiwa na alama 29 ikiwa imecheza michezo 11.

Mchezo unaofuata Yanga itaikaribisha Mbeya City katika Dimba la Benjamin Mkapa Novemba 26, 2022

yangasc-316350820-1260279921418252-3466976037185381850-n yangasc-316359332-588518343045298-6611922461518301705-n yangasc-316653659-462400512667240-7291656690600273306-n

Soccer-Table-Graphic

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post