Na Deborah Boniface
Zoezi la ufanyaji usafi nchini limekuwa chachu ya maendeleo hasa katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama hasa katika maeneo ya masoko,hoteli,stendi za mabasi ,mashuleni na lengo kuu ni kuepukana na magoniwa hatarishi kama vile kichocho,kipindupindu n.k ambayo yamekuwa tishio kubwa kwenye jamii yetu.
Vijana WA eneo la goba ,jijini Dar es salaam, wameonyesha jitihada zao katika kuiunga mkono serikali ,kwenye zoezi la ufanyaji usafi uliofanyika goba Leo hii, "usafi ni muhimu kwenye maisha yetu hasa katika maeneo tunayoishi,na maeneo tunayofanyia kazi,na lengo kuu ni kupunguza maambukizi ya magoniwa ya mlipuko yanayosababishwa na uchafu"alisema Ruben.
Kutokana na agizo la serikali katika kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa safi na salama,kumekuwa na miamko mbalimbali ,zikiwemo taasisi,makampuni,vikundi mbalimbali ambavyo vimekuwa vikitekeleza agizo Hilo ikiwemo ufanyaji WA usafi katika baadhi ya maeneo ,kama vile hospitali,sehemu za fukwe ,masokoni.
Jamii inashauriwa kutunza mazingira na kuyaweka safi na salama ili kuepusha maambukizi ya magoniwa ,na pia kuyapendezesha mazingira yetu kuwa safi na salama wakati wote,hasa katika maeneo muhimu ,hasa kwenye kusaidia kutangaza vivutio vya kitalii nchini mwetu.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.