Refa Mike Dean amepewa adhabu ya kushushwa daraja hadi katika ligi ya daraja la kwanza kutokana na kutoa maamuzi mabovu kwenye baadhi ya michezo aliyowahi kuchezesha kwenye mechi za ligi kuu ya Uingereza.
Mara kadhaa refa huyo amekuwa akilalamikiwa kuwa na maamuzi mabovu katika mechi anazochezesha. Mechi ambazo Dean analalamikiwa kuzitolea maamuzi mabovu ni ile ya West Ham United dhidi ya Manchester United baada ya kumpa kadi nyekundu ya kimakosa Sofiane Feghouli pamoja na kukubali goli la kuotea la Zlatan Ibrahimovic.
Mechi nyingine anazolalamikiwa ni pamoja na Everton dhidi ya Liverpool iliyochezwa Disemba 19 mwaka jana ambapo alionekana kuibeba zaidi Everton kutokana na kushindwa kutoa kadi nyekundu kwa Ross Barkley baada ya kumchezea rafu mbaya Jordan Henderson.
Mechi nyinyine ambazo alizoharibu refa huyo ni Tottenham dhidi ya Aston Villa na Stock City dhidi ya Sunderland.

Dean ambaye amechezesha mechi za ligi kuu kwa misimu 17 atachezesha mechi yake ya kwanza ya Championship Jumamosi hii watakapokutana mahasimu kati ya Barnsley dhidi ya Leeds.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.