Unknown Unknown Author
Title: NGUBIAGAI ANUSA UZEMBE KATIKA UKUSANYAJI NA MATUMIZI YA MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Kilwa Masoko. Kiwango kidogo cha fedha zinazokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya ...
Na. Ahmad Mmow, Kilwa Masoko.
Kiwango kidogo cha fedha zinazokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi. Kimesababisha mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai kuomba taarifa za mapato na matumizi ya fedha ya kila mwezi.
Christopher Ngubiagai
DC Christopher Ngubiagai akitoa maelekezo

Ametoa kauli hiyo katika vijiji vya Malendego na Njianne alipozungumza na watumishi wa kizuizi cha Malendego na kituo cha afya cha Tingi. Ngubiagai alisema kunahaja ya kufuatilia kwa karibu mapato na matumizi ya fedha hizo na njia zinazotumika kukusanya mapato ya halmashauri hiyo kutokana na mwenendo usioridhisha wa ukusanyaji na matumizi ya mapato ya halmashauri unaotishia uwepo wa halmashauri hiyo.

Alisema lengo kubwa la uamuzi wake huo ni kujiridhisha kama waliopewa dhamana ya kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo vya ndani wanawajibika ipasavyo au niwazembe wanaositahili kuachia ngazi.

DC Ngubiagai ambae anafanya ziara ya kikazi katika vijiji vya wilaya hiyo alionesha wasiwasi mkubwa kuhusu uadilifu na uaminifu wa wanaokusanya mapato. Kutokana na kiasi kisichoridhisha cha 34% kinachokusanywa kati ya 80% kinachotakiwa kukusanywa kila mwaka kwa mujibu wa sheria.

Alisema licha ya kuwanakiwango kidogo cha mapato ya ndani kinachokusanywa, hata matumizi ya fedha zinazotokana na mapato hayo hayaridhishi. Akibainisha kuwa zinatumika kulipa posho za madiwani na safari za watumishi. Badala ya kutumika kwa mambo ya msingi na muhimu.
"Watumishi hawapati mafunzo sababu hakuna fedha, vifaa vya ofisi havinunuliwi. Hata samani na vifaa vya ofisi havinunuliwi na kompyuta hazitengenezwi, unaambiwa hakuna fedha. Lakini waheshimiwa madiwani hawadai na wanalipwa posho kwa wakati na posho za usafiri hazikosekani," alisema Ngubiagai.

DC huyo alionya kuwa baadhi ya watumishi atawatumbua kwasababu anawajua na siku zao za kuwa watumishi wa umma zinakaribia kwisha. Akibainisha kwamba halmashauri inaposhindwa kufikia lengo inalojiwekea ni ushahidi unaothibitisha kunaudhaifu katika mifumo ya ukusanyaji mapato au kunawatendaji wanahujumu mapato yanayokusanywa.
"Gari iliyo na mazao yaliyonunuliwa na kusafirishwa kwa magendo inawezaje kufika na kushikwa Vikindu wakati barabarani kunavizuizi, ni dhahiri kunamchezo mchafu unafanyika, mzigo wenye uzito wa tani kumi unalipiwa uzito wa tani tatu pananini hapa," alieleza na kuhoji Ngubiagai.

Alitahadharisha kwamba hali hiyo isipo dhibitiwa kunauwezekano mkubwa wa halmashauri hiyo kufutwa, kwa kuzingatia kwamba sheria inataka halmashauri iweze kukusanya mapato kutoka katika vyanzo vyake vya ndani sio chini ya 80% ya lengo.

Hata hivyo halmashauri hiyo kutoka mwezi Julai hadi Desemba mwakajana ilikusanya asilimia thelathini na nne tu.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top