Unknown Unknown Author
Title: KITUO CHA AFYA TINGI WAJIFUNGULIA KWA KUTUMIA TOCHI, TATIZO LA UMEME NA MAJI NI DONDA NDUGU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow. Kilwa Kituo cha afya cha Tingi wilayani Kilwa kinakabiliwa na matatizo lukuki ambayo ufumbuzi wake ni kitendawili kigumu....
Na. Ahmad Mmow. Kilwa
Kituo cha afya cha Tingi wilayani Kilwa kinakabiliwa na matatizo lukuki ambayo ufumbuzi wake ni kitendawili kigumu.
Kituo cha afya cha TingiKituo hicho chenye uwezo wa kulaza wagonjwa kumi kwa wakati mmoja na kinachotegemewa na vijiji takribani 14 kinakabiliwa na tatizo la umeme huku kikilipa ankara kubwa isiotokana na matumizi ya kituo hicho.

Akizungumza kwa masikitiko mbele ya mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai, msimamizi wa kituo hicho, ofisa muuguzi Mwanaisha Manzi. Ameeleza kuwa wanalazimika kuzima umeme kila saa mbili asubuhi kila siku na kuwasha saa mbili usiku ilikukwepa kulipa ankara kubwa ambayo haitokani na hailingani na matumizi ya kituo hicho.

Alisema kila siku wanatumia Tsh 10,000.00 sawa na Tsh 300,000.00 kila mwezi kwa malipo ya umeme ambayo hayalingani na matumizi halisi kwa siku.
"Muda mwingine tunalazimika kutumia tochi tunapowahudumia wajawazito wakati wanajifungua". Mwanaisha alisema 

Baada ya kufuatilia kwa maofisa wa TANESCO waliambiwa ankara hiyo haitokani na matumizi pekee ya kituo hicho. Bali wanalipia deni la mtu mwingine aliyepo nje ya wilaya ya Kilwa na mkoa wa Lindi.
"Tuliambiwa bila kuwa wafuatiliaji wazuri tusingebaini tatizo hilo kwani hali hiyo inawakumba watu wengi lakini kutokana na kutokuwa makini hawajui na wanaendelea kuumia, wanasema madeni yakuwa makubwa na watumiaji wanashindwa kulipa shirika linamtupia deni hilo mtu yeyote alipe," alisema. 

Muuguzi Mwanaisha aliongeza kubainisha kwakusema pamoja na juhudi kubwa ya kutaka kasoro hiyo irekebishwe. Ikiwa na kufikisha malalamiko kwa mamlaka mbalimbali lakini juhudi hizo hazijafanikiwa kuondoa tatizo hilo ambalo limedumu kwa miaka mitatu.

Pamoja na tatizo hilo muuguzi huyo alisema kituo hicho kinatatizo sugu la maji ambalo limedumu kwa takribani miaka 40.
"Kila siku tunatumia Tsh 6,000.00 kununua maji, dumu moja la maji tunanunua kwa Tsh 400.00," alisema.

Kutokana na hali hiyo muuguzi Mwanaisha ameeleza kuwa akinamama wajawazito wanaokwenda kujifungulia kwenye kituo hicho wanalazimika kwenda na maji.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya Ngubiagai licha ya kutaka TANESCO iondoe mita iliyopo na kuwekwa nyingine. Aliahidi kufuatilia ili pesa zilizolipwa na kituo hicho kwa ajili ya madeni ya watu wengine zinarejeshwa.
"Wakati tunafuatilia fedha hizo mita hii iwe imebadilishwa, haiwezekani hali hii iachwe inaendelea. Kesho saa mbili asubuhi wewe DAS, meneja wa TANESCO na mimi tukutane ofisini kabla sijaanza safari ya kuendelea na ratiba ya ziara yangu," alisisitiza Ngubiagai.

Meneja wa TANESCO wa wilaya ya Kilwa, James Chinula, alisema shirika lake limeshachukua hatua katika kuondoa tatizo hilo ambalo lilisababishwa na urekebishaji mfumo. 
Katika kuondoa mita za zamani na kuweka mita za LUKU.

Ambapo kituo hicho kimepewa uniti 6000 kufidia malipo yaliyofanywa na kituo hicho kinyume na matumizi halisi. Alibainisha kwamba kituo cha afya cha Tingi kilikuwa hakitumii mita za mfumo wa zamani. Hivyo hakikuwa na deni.
"Shirika halina utaratibu wakuwalipisha madeni wateja wasio na madeni ili kufidia madeni ya wengine, kwahiyo kituo hicho hakikulipishwa wala kubambikiwa madeni ya wateja wengine," alisema Chinula.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top