Unknown Unknown Author
Title: DC AKUNJUA MAKUCHA ATOA SIKU SABA KWA WATOTO WASIO RIPOTI SHULENI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea Kiwango kidogo cha watoto walioripoti katika shule za sekondari wilayani Nachingwea, kimemlazimisha mkuu wa wi...
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea
Kiwango kidogo cha watoto walioripoti katika shule za sekondari wilayani Nachingwea, kimemlazimisha mkuu wa wilaya hiyo, Rukia Muwango kutoa siku saba tu kwa wazazi na walezi wa watoto ambao hadi sasa hawajaripoti shuleni.Wanafunzi
Muwango ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, alitoa agizo hilo juzi katika kijiji cha Ruponda wakati anazungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.

Alisema hali ya mahudhurio ni mbaya, hasa kwa watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.

Hivyo yeye kama msimamizi mkuu wa shuguli za maendeleo katika wilaya hiyo hayupo tayari kuona wala kusikia hali hiyo inaendelea.

Hivyo ametoa siku saba kuanzia juzi wazazi na walezi wa watoto hao wahakikishe wanaripoti shuleni. Huku akihaidi kuto muonea haya wala huruma mzazi na mlezi yeyote atakae puuza agizo hilo. Bali hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Alisema kati ya wanafunzi 2070 waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka huu, ni wanafunzi 451 tu walioripoti hadi sasa. Ikiwa namaana hadi sasa watoto 1619 hawajaripoti.

Muwango amewataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuandaa sababu zinazohalalisha uzembe uliofanyika. Badala yake watekeleze agizo hilo, kwasababu walikuwa na muda wa kutosha wa kufanya maandalizi.
"Kisingizio cha kutolipwa fedha za mauzo ya korosho hakina nafasi kwasababu wakulima wengi mmeshalipwa, wasiolipwa ni wale wachache ambao korosho zao ziliuzwa katika mnada wa nane na tisa bali minada mingine yote imelipwa," alisema Muwango.

Katika kuonesha hakuwa anafanya masihara na wananchi hao kuhusu agizo lake, mkuu huyo wa wilaya ameruhusu watoto waliochaguliwa na hawana sare wakaripoti na kutumia sare zao za shule za msingi. Bali watavaa ndani ya wiki moja ambayo wazazi na walezi wao watatumia kukamilisha maandalizi.

Alionya pia tabia ya wazazi kushiriki kwa makusudi kuwachelewesha watoto kuripoti kwawakati. Alisema tabia hiyo nisawa na kujenga msingi wa matokeo mabaya ya ufaulu. Hivyo hawayupo tayari kuona hali hiyo inatokea katika wilaya anayoiongoza.
"Nimeteuliwa na kuletwa hapa pamoja na mambo mengine ya kiutawala na uongozi nipamoja na kusimamia maendeleo ya wananchi, kwahiyo nitakapoacha hali hii iendelee nitakuwa sitoshi na nitakuwa nimemuangusha na hata kumfedhehesha akiyeniteua," alisema Muwango.

Mbali na agizo hilo amewataka wananchi wilayani humo kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na vyakula. Huku akiwambusha hali ya ukame ambayo imeanza kuonekana.

Hivyo hawana budi kununua chakula pindi wanapolipwa fedha zao za mauzo ya korosho. Alisema hali ya ukame iliyoanza kuonekana inatakiwa ichukuliwe tahadhari kubwa na kila mmoja. Ikiwamo kupunguza matumizi yasio ya lazima ya chakula.
"Lakini pia pandeni mazao yanayokomaa kwa muda mfupi na yanayohimili ukame, punguzeni sherehe zinazohitaji matumizi makubwa ya vyakula," alisisitiza Muwango.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wawilaya miongoni mwa shule ambazo zimekuwa kinara wa watoto waliochaguliwa kushindwa kuripoti ni pamoja Ruponda, Nditi, Mkutokuyana, Lionja na Ndomoni.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top