Unknown Unknown Author
Title: ASILIMIA 78.21 YA WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA NACHINGWEA, WASHINDWA KURIPOTI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea. Wanafunzi 1619 waliochaguliwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu katika shule mbalimbali za sekonda...
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.
Wanafunzi 1619 waliochaguliwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu katika shule mbalimbali za sekondari wilayani Nachingwea bado hawajaripoti.
Wanafunzi wa Sekondary
Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya hiyo, Rukia Muwango alipozungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalibali ofisini kwake mjini Nachingwea. 

Muwango ambae ametoa wiki moja kwa wazazi na walezi wenye watoto wahakikishe wameripoti shuleni, amesema kati ya watoto 2070 waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza watoto 1619 sawa na 78.21% hawajaripoti shuleni.

Ambapo watoto 451 sawa na 21.79% tu ndio walioripoti shuleni. Alisema licha ya watoto hao wanaotakiwa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu, lakini pia watoto wengi wanasoma madarasa mengine hawajaripoti.

Alisema wazazi na walezi watoto hao hawana sababu za msingi zinazosababisha watoto wao washindwe kuripoti hadi sasa.
"Nimetembea nakukutana na wazazi katika tarafa zote zinazounda wilaya hii, lakini wameshindwa kunieleza sababu za msingi zinazosababisha hali hiyo," alisema Muwango.

Mkuu huyo wa wilaya alisema wazazi na walezi walikuwa na muda wa kutosha kufanya maandalizi baada ya kusikia watoto wao wamechaguliwa kuendelea na masomo. Hata hivyo wameshindwa kutumia muda huo.

Kutokana na hali hiyo mkuu huyo wa wilaya ametoa siku 17 kuanzia tarehe 15 mwezi huu wahakikishe watoto wao wanakwenda shuleni. Alibainisha kwamba kwa jinsi serikali ilivyobeba jukumu kubwa ili watoto wote wanachguliwa wanakwenda shuleni. Alitaja baadhi ya majukumu hayo kuwa ni watoto kuanzia shule ya msingi hadi sekondari kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne wanasoma bila malipo, nyumba za walimu zipo, mishahara wanalipwa na serikali.

Hivyo hawana sababu ya kushindwa kupeleka watoto wao. Alizitaja baadhi ya shule ambazo watoto wengi hawajaripoti ni :
  1. Kigei ambayo waliochaguliwa ni 66, walioripoti ni 5. 
  2. Nditi waliochaguliwa 35 walioripoti ni 7.
  3. Ruponda waliochaguliwa ni 54 walioripoti ni 2.
  4. Lionja 61 aliyeripoti ni 1. 
  5. Namapwia 24 aliyeripoti 1.
  6. Kipara 39 walioripoti 2.
  7. Mkotokuyana 28 walioripoti 4.
  8. Ndomoni 85 walioripoti 3.
  9. Namatula ni 35 walioripoti 3.
Hata hivyo baadhi ya wazazi wamesema hali hiyo imesababishwa na kutolipwa fedha za korosho zao za msimu wa 2016/2017 ambazo wameuza kuanzia mwezi oktoba mwaka jana hawajalipwa.

Ingawa mkuu huyo wa wilaya alisema wakulima wengi wamelipwa bali hawakufanya maandalizi kuhusu kuwanunulia watoto wao mahitaji muhimu ya shule. Bali mwitikio mdogo wa wazazi kuhusu elimu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top