Unknown Unknown Author
Title: AJUZA AMWAGA CHOZI KULILIA MALIPO YA KOROSHO ALIZOUZA MWAKA JANA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow. Kuchelewa kwa malipo ya wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo hivi karibuni ilitajwa na baadhi ya vy...
Na. Ahmad Mmow.
Kuchelewa kwa malipo ya wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo hivi karibuni ilitajwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba wakulima wa zao hilo wamepata fedha nyingi nakusababisha kuwanywesha mbuzi soda, kumegeuza furaha hiyo na kusababisha vilio.
Crying Woman
Katika tikio la hivi karibuni linalodhihirisha ucheleweshaji malipo hayo unasababisha mateso kwa wakulima wa zao hilo.

Kikongwe anayetambulika kwa jina la Joyce Choaji anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 80, mkazi wa kijiji cha Kilimarondo wilaya ya Nachingwea, juzi alimwaga machozi mbele ya waandishi wa habari waliokwenda kijijini hapo.

Ajuza huyo ambae alipeleka korosho zake mwezi Novemba mwaka jana na hajalipwa hadi sasa, aliangua kilio na kusema alikuwa hajala chakula kwa muda wa siku mbili na alikuwa hana uhakika kama atakula.

Kwamadai kwamba hata wasamaria wema waliokuwa wanamsaidia wapo hoi na wamechoka kumsadia. Alisema matarajio yake yalikuwa alipwe malipo ya korosho ndipo anunue chakula.

Hata hivyo hajalipwa na hajui atalipwa lini. Alisema hali hiyo inawakabili watu wengi kijijini hapo, na wote matarajio yao yalikuwa kwenye korosho.
"Mimi naishi peke yangu wala sina mtoto, hapa nilipo sina nguvu pamoja na uzee nilionao siku ya pili leo sijakula chochote. Serikali mtuonee huruma sisi masikini hatujakosea chochote korosho tulipata lakini mumechukua mnatuacha tunakufa kwa njaa,'' alisema ajuza huyo huku akidondosha machozi. 

Huku akionesha stakabadhi za mauzo bibi Joyce alisema alipeleka ghalani korosho zake zenye uzito wa kilo 158 tarehe 25 mwezi Novemba mwaka jana, lakini hajalipwa na kuwa chanzo cha mateso anayopata.

Kwa madai kwamba kiasi cha fedha ambazo angelipwa kingetosha kununua chakula ambacho kingemtosha kwasababu anaishi peke yake.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Anjelous Ng'oloko alisema hali ya chakula katika kijiji hicho na tarafa nzima ya Kilimarondo ni mbaya. Kwasababu mwaka jana mazao yaliharibiwa na mvua. Hivyo matarajio yao yakuokoka na njaa yalikuwa kwenye korosho. Hata hivyo hawajalipwa.

Mwenyekiti huyo alisema hali hiyo inasababisha baadhi ya wakulima kuweka madukani stakabadhi za mauzo ya korosho zao kama dhamana ili wapate chakula.
"Unga unauzwa bei za juu, kama ukikopa inabidi ulipe riba ambayo ni nusu ya bei unaouziwa, ukikopa shilingi laki moja taslimu itakubidi ulipe shilingi laki mbili, stakabadhi ndio dhamana yako," alisema Ng'oloko.

Mkuu wa wilaya hiyo, Rukia Muwango licha ya kustushwa na taarifa hiyo na kuhaidi kuifanyia kazi ili kunusuru maisha ya wananchi hao, lakini alishangaa kusikia wakulima wengi hawajalipwa. Wakati aliambiwa fedha za wakulima zilishapelekwa kwenye vyama vya msingi.

Alisema ingawa korosho nyingi katika maeneo hayo huvunwa na kufikishwa maghani mwishoni kutokana na hali ya hewa. Lakini hakutarajia kusikia wakulima wengi hawajalipwa.

Muwango alibainisha kwamba minada ambayo fedha zake hazijalipwa ni mnada wa nane na tisa. Hivyo ikibainika wakulima hao hawajalipwa kutokana na uzembe wawatendaji wa vyama vya ushirika atashugulika na watendaji hao waliosababisha mateso kwa wakulima.

Meneja wa chama kikuu cha ushirika cha Runali, Christopher Mwaya alisema vyama vya msingi vya ushirika vilishapewa fedha za wakulima kuanzia mnada wa kwanza hadi wa saba. Ambapo mnada wa nane na tisa malipo yake yataanza kutolewa leo.

Akibainisha kwamba sababu za wakulima kuchelewa hazitokani na uzembe wachama hicho. Bali sababu nyingi zipo juu ya uwezo wao. Ikiwamo makapuni yaliyo shinda zabuni kuchelewa kulipa na changamoto zilizotokana na mfumo mpya wa malipo ya zao hilo.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM

Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top