Unknown Unknown Author
Title: WAZAZI KILWA WAELEZA SABABU ZA UFAULU HAFIFU WILAYANI HUMO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Kilwa Masoko . Tabia ya baadhi ya wananchi ya kutohudhuria mikutano, imetajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazochangia ...
Na. Ahmad Mmow, Kilwa Masoko.
Tabia ya baadhi ya wananchi ya kutohudhuria mikutano, imetajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazochangia matokeo mabovu ya viwango vya ufaulu katika shule za msingi wilayani Kilwa.
Wanafunzi Shule ya Msingi
Hayo yalielezwa jana, mjini Kilwa Masoko na washiriki wa semina ya wadau wa elimu wa wilaya hiyo,wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya utafati ya mradi wa uahamasishaji wa utoaji wa elimu bora kwa kutumia rasilimali za ndani. Iliyoandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania (TANMET) kwa kushirikiana na wadau wengine kwa ufadhili wa shirika la misaada la Norway (NORAD).

Washiriki hao wakiwamo wazazi, wajumbe wa kamati za shule, viongozi wa serikaliza vijiji na kata, walisema wananchi wengi hawahudhurii mikutano na vikao vinavyotumika kujadili, kuibua miradi na kupanga mikakati ya maendeleo. Hali ambayo inasababisha matokeo mabovu ya viwango vya ufaulu kwa shule zilizopo wilayani humo. 

Walisema kama wananchi wengi wangekuwa wanahudhuria mikutano na vikao vya wazazi shuleni wangeweza kupata njia za kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu na nyingine za kijamii. 

Mzazi, Omari Mkuluwili, ambae pia ni mtendaji mkuu wa mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali wilayani Kilwa (KINGONET), alisema wananchi wengi hawahudhurii mikutano mikuu ya vijiji na vikao vya wazazi kwenye kamati za shule. Hali ambayo imasababisha washindwe kutoa michango yao ya mawazo katika kutengeneza mikakati ya kuzikabili changamoto za maendeleo na huduma za jamii. Ikiwamo zilozopo kwenye shule zao.
Wazazi Kilwa
Alisema kutokama na hali hiyo baadhi ya vijiji vinakabiliwa na matatizo ambayo wananchi wake wangekuwa wanashiriki na kuhudhuria vikao na mikutano mikuu na vikao mbalimbali yasingekuwepo.
"Kijiji fulani tulikosa watu kwenye mkutano, hata walipofuatwa walikataa kuja, nawachache waliokuwepo walikataa kusaini kitabu cha mahudhurio, ingawa lengo letu lilikuwa kuwaomba waibue mradi. Hata hivyo hatukufanikiwa na kijiji kile kinaendelea kuwa na tatizo la uhaba wa maji," alisema Mkuwili.

Mzazi huyo alibainisha kwamba wananchi wanahudhria na kujaa kwenye mikutano nipale wanapotaka kuwakataa na kuwaondoa viongozi wa vijiji au watendaji wao. Mjumbe wa kamati ya shule ya msingi ya Chumo, Zaria Said, alisema tabia ya wananchi kutohudhuria mikutano na vikao inachangia matokeo mabovu ya ufaulu. Kwasababu mikutano hiyo inatumika kuwakutanisha nakufanya majadiliano ya kutatua changamoto mbalimnali.

Mjumbe huyo alitolea mfano kijiji chake cha Chumo. Kwamba mikutano mikuu miwili ya kijiji haikufanyika kwasababu ya kukosa majidhurio. Kwahiyo ilihairishwa na aufahamiki nisiku gani utafanyika.

Nae mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Kikanda, Alli Komba, ambae mwaka jana shule yake ilifaulisha wanafunzi wote waliohitimu darasa la saba. Alikiri kuwa vikao na mikutano inamchango mkubwa wakuongeza viwango vya ufaulu iwapo wananchi wanahudhuria na kushiriki vikao na mikutano.

Komba alitolea mfano shule yake hiyo ambayo pamoja kuwa inamiundo mbinu mibovu lakini wanafunzi wanafanya vizuri darasani.
"Kinachochangia wanafunzi wanafaulu katika shule yetu niwazazi na walezi kukubali kuhudhuria na kishiriki vikao vya kamati ya shule," alisema Komba.

Mwenyekiti huyo licha ya kukiri kuwa hata katika kijiji cha Kikanda mahudhurio ya wananchi katika mikutano mikuu, lakini kwa kuwatumia wazazi na walezi wenye watoto wanasoma waliweza kupata njia mzuri za kutatua changamoto zilizokuwepo.

Mtemdaji wa kijiji cha Kibata, Mshamu Kipengele, alisema mtazamo kuhusu sera ya elimu bure imesababisha baadhi ya wazazi kuacha kuchangia wala kuhudhuria vikao vya kamati ya shule. Kwasababu wanaamini kila kitu kitafanywa na serikali. Hivyo hata uwahamasishaji wananchi wachangie michango kuhusu maendeleo ya shule umekuwa mgumu.

Kwaupande wake mwasilishaji wa utafiti huo kutoka shirika la ActionAid, Jacob Kateri, alisema matokeo ya utafiti uliofanyika yanaonesha katika shile 14, kamati za shile 10 na wazazi wa shule 10 walikiri kushiriki kusimamia bajeti za shule.

Kateri alibainisha kuwa kwakiasi kubwa watu walihojiwa katika makundi yote walikiri kuwepo kwa matokeo chanya ya uwepo wa ushirikishwaji wa wazazi kwenye kamati. "Kuchangia fedha na nguvu kazi kwa ajili ya miundombinu ya madarasa, nyumba za walimu na vyoo katika 4 za Masoko, Kibata, Lihimalyao Kusini na Somanga, kufuatilia maendeleo ya taaluma kulipelekea kuongezeka kwa ufaulu katika shule 4 za Kikanda, Kinjumbi, Njinjo na Migeregere, kuimarisha ustawi na afya za watoto katika shule 2 za Chuo na Njinjo," alisema Kateri.

Wadau wautekekelezaji wa mradi huo wa uhamasishaji wa utoaji elimu bora kwa kutimia rasimali za ndani ni ActionAid, Mtandao wa elimu Tanzania (TANMET) Mtandao wa mashirika yasio ya kiserikali katika wilaya (KINGONET), Shirika la maendeleo ya elimu Mtinko (MEDO) na Chama Cha Walimu Tanzania (CWT). Ambapo shule 15 zilihusishwa na utafiti huo.
*********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top