Unknown Unknown Author
Title: WANANCHI WA NANGANGA WAOMBA WAPELEKEWE ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Lindi. Baadhi ya viongozi na wananchi wa kijiji cha Nanganga wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi, wameiomba serikali kupelek...
Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Baadhi ya viongozi na wananchi wa kijiji cha Nanganga wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi, wameiomba serikali kupeleka vijijini elimu kuhusu haki za binadamu ili kupunguza migogoro inayotokana na kugombea mirathi na ardhi.
Wananchi
Picha kutoka Maktaba
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi kijijini hapo. Ikiwa ni mikutano maalum ya wiki ya sheria duniani, inayoratibiwa na kusimamiwa na shirika la msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto katika mkoa wa Lindi (LIWOPAC) katika mkoa huu kwa ufadhili wa sekretarieti ya msaada wa sheria.

Wananchi na viongozi hao walisema kuna umuhimu mkubwa wa elimu inayohusu haki za binadamu kufikishwa vijijini ambako nako kunamigogoro mingi. Hasa inayohusu mirathi na ardhi.

Walisema vijijini hakuna wanasheria ingawa kuna migogoro. Hivyo wananchi wamejikuta wakiingia kwenye migogoro ambayo ingeweza kuepukwa iwapo wangepata elimu hiyo.

Mwananchi Mustafa Hokororo alisema katika kijiji hicho kuna migogoro ambayo kama wananchi wangekuwa na elimu isingekuwepo. Akibainisha kuwa kutokana na wananchi
wengi kutokuwa na elimu wamejikuta wanadhulumiana na kusababisha migogoro na uhasama.

Mwananchi mwingine, Mwanahawa Hamisi, alisema kutokuwa na elimu kunasababisha washindwe kudai haki zao. Ikiwamo haki ya kutibiwa bure kama ilivyoagizwa na serikali kuwa watu wenye umri wa unaoanzia miaka 60 watibiwe bure.

Hata hivyo agizo hilo halizingatiwi na walikuwa hawajui kwamba hiyo ni haki yao na wanasitahili kudai.
"Kama tungekuwa tunapata elimu kama iliyokuja leo, tusingedhulumiana. Mirathi sisi wanawake tunadhulumiwa hatuna mtetezi, kwahiyo serikali ione umuhimu wa kufikisha elimu kama mlivyofanya nyinyi(LIWAPAC)," alisema Mwanahahawa.

Ofisa mtendaji wa kijiji hicho chenye kaya 700 na wakazi takribani 7000, Kassim Kambona, alisema kunaumuhimu kwa wananchi kupelekewa elimu mara kwa mara ili kupunguza migogoro inayoweza kuepukika. Akibainisha kuwa katika kijiji hicho kunamigogoro ya mara kwa mara inayotokana kugombea mirathi na ardhi.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Yustis Nachingulu, licha ya kuiomba serikali kuangalia namna ya kupeleka elimu vijijini, lakini pia aliiomba iwapelekee na kukiingiza kijiji hicho kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kupunguza kesi za ardhi kuhusu mipaka ya mashamba.

Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa waathirika wakubwa ni wazee na wanawake. Kwa upande wake, mkurugenzi wa LIWOPAC, Cosma Bulu, alitoa wito kwa wananchi hao kuzitambua na kudai haki zao kwa kuvitumia vituo vya msaada wa kisheria ambavyo vipo kwa ajili yao na vinatoa huduma za msaada wa kisheria bila malipo.
***********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top