Unknown Unknown Author
Title: LIWOPAC KUFUNGUA VITUO KWENYE KATA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Kilwa. KATIKA kuhakikisha jamii inazitambua haki zake za msingi na zabinadamu. Shirika la msaada wa kisheria kwa wanawak...
Na. Ahmad Mmow, Kilwa.
KATIKA kuhakikisha jamii inazitambua haki zake za msingi na zabinadamu. Shirika la msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto Lindi (LIWOPAC) limepanga kusogeza huduma zake hadi kwenye ngazi ya kata.
mama na mtoto
Hayo yalielezwa jana mjini Kilwa Masoko wakati wa mdahalo wa mradi wa OKOA MAISHA YA MTOTO MCHANGA KWA MAENDELEO ENDELEVU LINDI uliojikita katika kulinda haki ya binadamu ya kuishi.

Kwa kuwafanya wananchi waishio vijjijini wanakuwa na uelewa juu ya changamoto zinazo sababisha vifo vya watoto wachanga wenye umri wa kuanzia siku 0 hadi 7.

Akizungumza kwenye mdahalo huo, mkurugenzi wa shirika hilo, Cosma Bulu, alisema kunahaja ya kusogeza huduma za msaada wa kisheria katika ngazi za chini ili jamii iwe na uelewa mpana wakulinda na kuzitambua haki zake za msingi nakuweza kuzidai pindi zinapokosekana.

Alisema kwakuzingatia umuhimu huo, shirika lake limepanga kufikisha huduma za msaada wa kisheria katika kila kata ya mkoa huu. Baada ya Kila wilaya kuwa na kituo cha msaada wa kisheria.

Alisema iwapo watafanikiwa kufungua kituo katika kila kata, jamii inayozunguka maeneo hayo itaweza kutumia vituo hivyo kupata msaada wa kisheria. Bulu aliongeza kusema iwapo huduma za msaada wa kisheria zitasogezwa karibu na jamii, kunauwezekano mkubwa kwa jamii yenyewe kutatua changamoto mbalimbali za kisheria.
" Enzi za nyuma wazee wetu wilikuwa na vikao vikiitwa moto wa jioni ambavyo vilikuwa vinatumika kutatua migogoro katika jamii, nasi kwa kusogeza huduma katika ngazi za chini lengo lake nikuzifanya kama vikao vya moto wajioni," alisema Bulu.

Mkurugenzi huyo alisema kuna umuhimu mkubwa wa kila mtu kuzitambua haki zake za msingi ili aweze kuzidai wakati anajua ni nini anakidai, nani anasitahili kudaiwa, niwakati gani na wapi zinapatikana na kutolewa.

Nae mratibu wa mradi huo, Pius Phinias alisema ingawa sera nyingi zimetungwa ili kusogeza huduma za afya kwa watoto na akinamama. Lakini bado kunachangamoto zinazosababisha vifo vya watoto na akinamama wajawazito. 

Nikutokana na jamii kukosa utambuzi na njia ya kuzuia vifo hivyo ambavyo vinaweza kuepukika iwapo jamii yenyewe itatumia njia sahihi za kumlinda mtoto. Ikiwamo kutumia vema vituo vya kutolea huduma za afya na uepuka mila potofu.
"Utumiaji wa sehemu zinazotoa huduma za afya ni mdogo, iwapo jamii itabadilika kunauwezekano mkubwa wa kutokomeza tatizo hili," alisema Phinias.

Mratibu huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema watu wanaoshindwa kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa uzembe nakusababisha vifo vya watoto na akinamama wajawazito nisawa na wauwaji wengine wanao fanya mauji kwa kukusudia. Kwasababu vifo hivyo vinaweza kuepukwa. 

Kwa upande wake kaimu mkuu wilaya ya Kilwa, ambae ni katibu tawala wa wilaya hiyo, Haji Balozi, alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa taasisi za kiraia na mashirika yasio ya kiserikali katika maendeleo ya nchi na ustawi wa jamii.

Hivyo inajitahidi kufanya kazi kwa karibu na taasisi na mashirika hayo. Balozi alibainisha kuwa katika wilaya hiyo kunavitendo vya ukiukaji wa sheria na taratibu. Kutokana na baadhi ya watendaji kushindwa kuzingatia utawala bora.

Alisema baadhi ya watumishi wa umma wanatumia vibaya madaraka yao. Hivyo kusababisha ukikwaji wa misingi ya utoaji haki kwa mujibu wa sheria.
"Kuna baadhi ya watendaji wa vijiji na kata wanadiriki kufungua mashitaka ya kijinai badala ya polisi, kunahaja ya wananchi kupewa elimu ili wananchi wazitambue haki zao," alisema Balozi. 

Kaimu mkuu huyo wa wilaya aliliomba shirika hilo kusaidia kutoa elimu inayohusu ardhi. Kwasababu wilaya hiyo inamigogoro mingi inayohusu ardhi. Hivyo elimu kwa wananchi kuhusu ardhi ni muhimu sana.
********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top