VIONGOZI WA UPINZANI WAKAMATWA

Viongozi wa chama cha upinzani nchini Uturuki kinachowaunga mkono wakurdi cha HDP, wamekamatwa pamoja na wabunge wengine 9.
Lindiyetu Blog News
Selahattin Demirtas na Figen Yuksekdag, wanalaumiwa kwa kueneza propaganda kwa niaba ya wanamgambo wanaopigana vita na taifa la Uturuki.

Saa chache baada ya bwana Demirtas kukamatwa eneo la Diyarbakir, mlipuko wa bomu uliwaua watu wanane na kuwajeruhi wengine zaidi ya 100.

Wanamgambo wamekuwa wakipigana vita kwa miaka mingi wakitaka kupata uhuru wa wakurdi.
Uturuki
Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari lililipuka baada ya viongozi hao kukamatwa

Uturuki imesalia chini ya amri ya hali ya hatari ambayo ilitangazwa baada ya jaribio la mapinduzi lililotibuliwa mwezi Julai.

Amri hiyo inamruhusu Rais Recep Tayyip Erdogan na baraza lake la mawaziri kutotegemea bunge wakati wa kupitishwa sheria mpya na kufuta uhuru wa watu.

Serikali inasema kuwa wale waliokamatwa walitaka kufika kuhojiwa, ambapo pia waranti wa kukamatwa ulitolewa kwa wabunge wawili wa HDP ambao kwa sasa wako nchi za ng'ambo.

************

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post