Katika kesi inayomkabili msanii Judith Wambura Mbibo maarufu kama Lady Jay Dee dhidi ya walalamikaji Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba kesi namba 29 ya Mwaka 2013 hukumu yake imetolewa leo na Hakimu wa mahakama ya Wilaya Boniphace Lihamwike.
Kuwa wameridhishwa na ushahidi uliotolewa kuwa msanii huyo alitenda kosa la kuwadhalilisha na kuwakebehi kwa maneno machafu ndugu Joseph Kusaga pamoja na Ndugu Ruge Mutahaba.
Hivyo mahakama ya wilaya ya Kinondoni imeamuamuru msanii huyo kuomba radhi katika chombo cha habari cha kitaifa au kinachosikika kimataifa pamoja na duniani nzima kuwa maneno yake yalikuwa ya kashfa na udhalilishaji yenye lengo la kuichafua taswira nzuri ya ndugu Kusaga pamoja na ndugu Ruge Mutahaba vilevile Mahakama imemuamuru msanii huyo kulipa fidia na gharama za uendeshwaji wa kesi hiyo.

Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa leo saa mbili na Nusu asubuhi katika mahakama ya wilaya kinondoni upande wa Msanii Judith Wambura uliwakilishwa na Wakili wake aitwaye Advocate Chacha licha ya msanii huyo kuhudhuria mahakamani hapo na kushindwa kushuka kwenye gari aina ya Noah waliyokuwa wamefika nayo Mahakamani hapo akiambatana na Meneja wake Seven Mosha ambaye alizuiliwa getini na walinzi kutokana na kuvaa nguo isiyozingatia maadili ya Mahakama.
Mwenendo wa kesi hiyo iliyofunguliwa tangu mwaka 2013 kwa msanii huyo akituhumiwa kuwatukana, kuwakebehi pamoja na kuwakashifu ndugu Joseph Kusaga pamoja na Ruge Mutahaba kupitia mitandao ya kijamii na mahojiano aliyokuwa akifanya mara kwa mara na vyombo tofauti vya habari.
Tangu kesi hiyo ilipofunguliwa msanii huyo amekuwa na mwenendo usiokuwa wa kuridhisha na kumfanya kushindwa kesi hiyo ni pamoja na;

- Kukosa ushahidi wa yale aliyokuwa akiyazungumza yeye binafsi kwamba ametendewa na kufanyiwa na washtaki.
- Kukosa mashahidi wa kusimama mahakamani kutetea alichokuwa anakisema kwani mpaka kesi inamalizika hakuweza kuleta shahidi hata mmoja. upande wa washitaki uliweza kuleta mashahidi takribani 15 mpaka hukumu ya kesi inasomwa hii Leo.
- Kutokuhudhuria mahakamani yeye mwenyewe, jambo linalotafsiriwa na wengi kama kutokuwa makini lakini pia kukurupuka kwa yale aliyokuwa akiyasema na kuandika kwani inawezekana kabisa sababu tajwa hapo juu zilimfanya aingie mitini.
*************
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.