Unknown Unknown Author
Title: DIAMOND AMCHANA LIVE OMMY DIMPOZI REDIONI CHEKI VIDEO HII HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Diamond amefunguka kuhusu jitihada zilizowahi kufanywa ili kumaliza bifu lake na Ommy Dimpoz. Ni muda mrefu wawili hao wamekuwa hawaele...
Diamond amefunguka kuhusu jitihada zilizowahi kufanywa ili kumaliza bifu lake na Ommy Dimpoz.
Diamond and Rich Mavoko
Ni muda mrefu wawili hao wamekuwa hawaelewani japo hakuna aliyewahi kuweka wazi chanzo cha ugomvi wao.

Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond amethibitisha kuwa aliwahi kutafutwa na Dimpoz pamoja na kuwatuma watu ili wayamalize.

“Kashatuma watu wengi sana, kashamtuma Sallam, alishanipigia mpaka na simu nikashindwa kupokea nitaongea naye nini,” alisema Diamond.

“Mipaka ilivuka halafu mimi ni muislam. Mimi sina matatizo na watu ndio maana wakijaribu kushindana na mimi huwa wanashindwa. Hata ukiniangalia sina hata pete ya kijani kwenye vidole vyangu,” aliongeza.

Diamond Vs Ommy Dimpoz
Hata hivyo wakati Diamond akihojiwa, Ommy Dimpoz alitweet kukanusha alichokisema.

“Aisee kumbe @Sallam_SK kila siku unavyonibembeleza tuyamalize na Mwana kumbe nakutuma kweli nyie profeshenooo ,” ametweet Ommy.

“Wazee @BDozen @CloudsMediaLive Naombeni Kipindi Kesho ,” ameongeza.

Wakati huo huo Sallam amemjibu Ommy: "Sijakuomba mie! Kumbuka aliyekwambia nani Na mie nilijibu nini? Hata wakati ulipokuja kuomba yaishe na mie kumbuka nani alikuleta!"

Bifu la Ommy na Diamond imeongezeka zaidi kuanzia jana baada ya kutoka kwa wimbo wa Rich Mavoko ‘Kokoro’. Wawili hao wametupiana vijembe kwenye Instagram.

HII HAPA FULL INTERVIEW. BOFYA PLAY

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top