DIAMOND PLATNUMZ BADO KURA CHACHE TU KUWA KINARA KATIKA TUZO HIZI

Hit Maker wa "Salome" na "Kidogo" Diamond Platnumz ni Miongoni mwa wasanii kutoka Tanzania wanao wania tuzo mbalimbali Barani Afrika na Marekani.
Diamond Platnumz
Hapa naomba nikupe halihalisi ilivyo katika Tuzo zijulikanazo kama AELAAWARDS ambazo Msanii Diamond Platnumz yupo katika Kipengele cha BEST COLLABORATION [AFRICA].

Katika Kipengele hicho anachuana na wasanii PAPA DENIS x KOREDE BELLO na wimbo wao WONDER ambao hadi sasa jamaa hawa wanaongoza kwa kura 16450 huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Diamond Platnumz kwa kupata Kura 13001 kupitia wimbo wake wa "KIDOGO" aliyowashirikisha mapacha kutoka Nigeria Peter na Paul OKOYE (P-SQAURE).

Mchuano ni mkali na kama wewe ni Mtanzania na unataka Msanii huyu ashinde Tuzo hiyo basi unatakiwa kumpigia KURA kwa nguvu zote ili aibuke kinara katika Kipengere hicho.

LINK YA KUPIGA KURA HII HAPA...BOFYA HAPA
****************

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post