Unknown Unknown Author
Title: DC AMTAKA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KILWA KUJIELEZA KUHUSU UKWAMAJI WA UKARABATI SHULE YA SEKONDARI KIPATIMU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow. Kilwa Masoko. Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai amemtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kil...
Na. Ahmad Mmow. Kilwa Masoko.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai amemtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, kumpa sababu za kukwama kwa ukarabati wa miundo mbinu ya shule ya sekondari ya kutwa ya Kipatimu.
wanafunzi
Ngubiagai alitoa agizo hilo juzi, alipotembelea shule hiyo kijijini Kipatimu. Mkuu huyo wa wilaya, alisema kunahaja ya kupatiwa maelezo na sababu za kukwama ukarabati huo, ikizingatiwa kwamba fedha kwa ajili ya kazi hiyo zilishapelekwa. 

Huku akibainisha shilingi 200.00 zilizotolewa na serikali kwa kazi hiyo zingetosha.Hata hivyo ujenzi umesimama na haileweki sababu nini na utaendelea lini.
"Kaimu mkurugenzi ndani ya wiki tatu andaa maelezo na unipatie ili niweze kujiridhisha, maana kazi imesimama kwa takribani miaka minne na sababu hazieleweki. Nataka nijue kiasi cha fedha zilizotumika na zilizobaki, sababu za kukwama kazi hii na mmepanga kuendelea na kumaliza lini," alisisitiza Ngubiagai.

Aidha, mkuu huyo wa wilaya alishauri halmashauri izishirikishe kikamilifu bodi za shule kwa kuzipatia taarifa kamili za miradi inayotekelezwa katika shule zake.

Akifafanua kwamba tabia ya kutozishirikisha bodi za shule inasababisha zishindwe kufuatilia na kusimamia kwa ukaribu miradi hiyo.

Awali mkuu wa shule hiyo yenye wanafunzi 262 na walimu 12, Mohamed Kalyoma, alisema shule hiyo ilikuwa ni miongoni mwa shule zizopata miradi ya ukarabati mkubwa wa miundombinu yake.

Mkuu huyo wa shule aliyataja maeneo ambayo yalitarajiwa kufanyiwa ukarabati huo ni vyumba kumi vya madarasa, ujenzi wa matundu nane ya vyoo vya wanafunzi na mawili ya vya walimu, kuvunja maabara chakavu moja na kukujenga upya, kuvunja jengo la utawala na kujenga jipya, kujenga tanki la maji na kuweka mfumo wa kuvuna maji ya mvua.

Mkuu huyo wa shule kwenye taarifa yake aliendelea kusema
"Kwa kuangalia tu kazi iliyofanyika ni sawa na 50% ya kazi yote iliyokusudiwa, ingawa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2011/2012 zilitenga shilingi 200.00 milioni kwa ajili ya kazi hiyo, na fedha hizo zilipelekwa kwa halmashauri ya wilaya hiyo kutoka serikali kuu. Hata hivyo ujenzi umekwama hadi leo na hazionekani juhudi zozote zinazofanyika kuondoa mkwamo huu ili kukamilisha ujenzi wa miundo mbinu iliyolengwa," alisema Mwalimu Kalyoma.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1990. Pia nimiongoni mwa shule 528 nchini, zilizoingizwa kwenye mpango wa MMES awamu ya pili, ambao ulipangwa ukamilike mwezi Juni mwaka huu. Kupitia mpango huo ilipatiwa mradi wa kufungiwa umeme kwenye majengo yake. Mradi ambao umekamilika na umeshakabidhiwa kwa shule hiyo.

Shule nyingine katika wilaya ya Kilwa zilizo kwenye mpango MMES awamu ya pili katika wilaya ya Kilwa ni Kikanda, Mpunyule na Ilulu.

Ikielezwa kuwa fedha za ukarabati mkubwa wa miundo mbinu ya shule ya sekondari ya kutwa ya Kipatimu ni za matumizi maalumu zilizotolewa na serkali kuu.
***********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top