Unknown Unknown Author
Title: TASAF NACHINGWEA WABAINI VIONGOZI WAZAMIAJI KWENYE MPANGO WA MALIPO KAYA MASKINI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea Zoezi la malipo kwa kaya maskini linalofanywa na mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) wilayani Nachingwea linalo...
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea
Zoezi la malipo kwa kaya maskini linalofanywa na mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) wilayani Nachingwea linalokwenda sambamba na kuwaondoa wasio nasifa limewakumba baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Nahimba.
TASAF
Wananchi wakiwa kwenye foleni ya malipo ya Kaya maskini yanayofanywa na mfuko wa TASAF.

Hayo yalibainika juzi baada ya maofisa wa mfuko huo wilayani humu kwenda kijijini hapo kufanya malipo kwa walengwa, kubaini wajumbe saba wa serikali ya kijiji hicho walikuwa wanufaika kinyume na utaratibu. 

Maofisa hao walioongozwa na ofisa ushauri na ufuatiliaji wa mfuko huo wa wilaya za Ruangwa na Nachingwea, Elias Muyomba walikwenda kijijini hapo ilikujionea zoezi la ulipwaji ruzuku kwa kaya maskini ikiwa ni mkupuo wa kumi na sita tangu mpango uanze kutekelezwa wilayani humu.

Wakati anawaomba wajumbe hao, Muyomba alisema wameanza kufuatilia kuwabaini watu wasio na sifa baada ya kusikia malalamiko kuwa baadhi ya watu hasa viongozi wa serikali za vijiji wameingia bila kukidhi vigezo.

Hivyo wanawaondoa na wataendelea na zoezi hilo ili wanaostahili waweze kuingizwa kwenye mpango huo.
"Kijiji hiki ni miongoni mwa vijiji ambayvyo viongozi wake wanalalamikiwa kujinufaisha na mpango huu, nilikuja na orodha ya majina na wenyewe wamekiri," alisema Muyomba.

Hata hivyo wajumbe wanne waliokuwepo kwenye mkutano huo, walisema wapo tayari kujiuzulu nafasi ya ujumbe wa kijiji iliwaendelee kuwa kwenye mpango huo.

Mjumbe Dalini Nyega alisema ameamua kujiuzulu kwa sababu vikao vya serikali ya kijiji havina posho. Hivyo aliona afadhali aendelee kuwa kwenye mpango huo ili apate fedha kila mwezi.

Nae Bakari kikope alisema ameamua kujiuzulu kwa sababu kabla ya kuchaguliwa kuwa wajumbe walikuwa kwenye mpango huo.
"Sisi tulikuwa kwenye mpango kabla ya kuwa wajumbe wa serikali ya kijiji, bora kuacha ujumbe maana kama mimi nategemewa ninafamilia kubwa, kwenye ujumbe hakuna ninacholipwa," alisema Bakari.

Akizungumzia kitendo hicho, Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango licha ya kuwapongeza maofisa hao kwa kuanza kuwabaini watu walioingizwa na kuingia kwenye mpango kinyume na utaratibu, ameagiza watu wote walioingia ama kuingizwa kwa mfumo usio rasmi na wasionasifa waondolewe.

Alisema wajumbe hao waserikali ya kijiji wanatakiwa kuondolewa na malipo yao yasitishwe mara moja.
"Hii inaonyesha huko vijijini taratibu zinakiukwa, viongozi wanatumia madaraka yao kujinufaisha, naagiza wajumbe hao na wengine watakaobainika hawana sifa waondolewe. Kama kuacha uongozi waache wakiwa wameshaondolewa," alisisitiza Muwango.

Jumla ya kaya 5730 zilizopo katika vijiji 69 kati ya 127 vilivyo katika wilaya hii zimefikiwa na kunufaika na mpango huo. ambapo takribani shilingi 2.5 bilioni zimetumika.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top