DIAMOND AFUNGUKA KILICHOMFANYA AMSAIDIE CHIDI BENZ, SOMA HAPA KUJUA.....

Msanii nyota wa bongo fleva nchini ,Diamond Platnumz amefunguka sababu inayomfanya awe mstari wa mbele kumsaidia Msanii Chid Benz ambaye hivi karibuni aliathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.
Diamond Platnumz
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa radio Diamond alielezea jinsi alivyokutana na Chid kwa mara ya kwanza na kumwomba kolabo kipindi ambacho Chid Benz alikuwa ana hit kila kona lakini hakumzungusha wala kumtoza hata shilingi kitu ambacho yeye anaona ni kikubwa sana kwake.
Chid Benz
“Mimi nilimwomba Chid Kolabo, kipindi hicho ana hit kila kona, hakunitoza hata shilingi kumi wala hakunizungusha hata kidogo, ndio maana linapokuja suala la Chidi nakuwa wa kwanza. Wakati namfuata Chidi,nikajua atanikatalia kwanza mimi mbana pua, lakini hakunizungusha na wala hakuniomba hata mia", alisema Diamond Platnumz.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post