NIJUZE NIJUZE Author
Title: TAARIFA YA KOFFI OLOMIDE KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 18 JELA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mwanamuziki maarufu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Koffie Olomide , adaiwa kuhukumiwa kifungo cha miezi 18 jela. Hukumu hiyo i...
Mwanamuziki maarufu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Koffie Olomide, adaiwa kuhukumiwa kifungo cha miezi 18 jela.
Koffie Olomide
Hukumu hiyo imekuja baada ya wiki iliyopita kusambaa kwa video inayomuonesha akimpiga teke dancer wake wakati wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa JKIA jijini Nairobi alikokuwa atumbuize Jumamosi iliyopita.

Tukio la kumpiga teke dancer wake limeteka vichwa vya habari duniani mwishoni mwa mwezi huu.

Kufuatia tukio hilo alifukuzwa nchini humo na show yake kusitishwa. Show nyingine aliyokuwa aifanye nchini Zambia ilisitishwa siku chache baadaye.

Kwa mujibu wa mtandao wa Voice of Congo, hukumu hiyo imependekezwa na mwanasheria mkuu wa serikali. Staa huyo alikamatwa nyumbani kwake wiki hii.

Japokuwa bado hakujatoka taarifa ya kina, imedaiwa kuwa hukumu hiyo haina faini ikimaanisha kuwa Olomide lazima aende jela.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top