NIJUZE NIJUZE Author
Title: KAMPUNI MPYA YA SIMU ZA MIKONONI YAANZA VIBAYA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Ni wazi kampuni mpya ya simu za mkononi ya Halotel imeanza vibaya mara baada ya kujaribu kutupa kete yake kwa watumiaji wa simu za mkononi...
Ni wazi kampuni mpya ya simu za mkononi ya Halotel imeanza vibaya mara baada ya kujaribu kutupa kete yake kwa watumiaji wa simu za mkononi Tanzania tangu kuzinduliwa kwake Oktoba 16 mwaka jana.
Halotel
Kampuni hiyo ambayo hadi sasa ina miezi tisa pekee tangu kuingia kwenye soko la ushindani huku ikijaribu kudonoa donoa wateja kutoka kwenye makampuni mengine imejikuta ikiingia kwenye kashkash ya kutozwa faini ya shilingi milioni 107 za Kitanzania baada ya kukiuka masharti ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 na Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Leseni za 2011.
Halotel
Aidha kampuni nyingine zilizotozwa faini na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kukiuka sheria ni pamoja na AIRTEL TANZANIA LIMITED sh. 182,500,000, BENSON INFORMATICS LIMITED maarufu kama Smart sh. 17,000,000,000, MIC TANZANIA LIMITED maarufu kama TIGO sh.189,000,000 na VODACOM TANZANIA LIMITED sh. 92,000,000.

Adhabu hizi zimetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 33 ya Kanuni za Leseni za mwaka 2011 zilizotolewa chini ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) na vifungu 93,130 na 131 vya Sheria hiyo na kifungu 93 (2,3 na 4) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010 na Kanuni ya 33 ya Kanuni za Leseni za 2011.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top