NIJUZE NIJUZE Author
Title: MEMPHIS HAJIAMINI KAMA ATABAKI MBELE YA MOURINHO, AANZA KUHAMA ENGLAND MAPEMAAA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo Mholanzi Memphis Depay hana uhakika kama ataendelea kubaki katika kikosi cha Manchester United chini ya Kocha mpya, Jose Mourinho . ...
Kiungo Mholanzi Memphis Depay hana uhakika kama ataendelea kubaki katika kikosi cha Manchester United chini ya Kocha mpya, Jose Mourinho.
Memphis Depay
Depay ameanza kuhamisha vita vyake kurudisha kwao nchini Uholanzi akianza na magari yake ya kifahari.

Gari lake la kifahari aina ya Mercedes G Wagon lenye thamani ya pauni 100,000 pamoja na pikipiki aina ya Scorpion yenye thamani ya pauni 13,500 pia zimepelekwa kwao Uholanzi.

Tayari kuna taarifa Mholanzi huyo mwenye miaka 22, alianza kusafirisha gari lake la kifahari zaidi aina ya Rolls Royce Wraith lenye thamani ya pauni 250,000 kulirejesha kwao Uholanzi. Hata hivyo, bado Mourinho bado hajatoa Orodha ya wachezaji watakaobakia au kuondoka clabuni hapo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top