NIJUZE NIJUZE Author
Title: JENEZA LA MUHAMMAD ALI LASWALIWA MAREKANI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Maombi ya Kiislamu ya kuswaliwa kwa jeneza la marehemu bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali yameanza hivi punde katika jimbo la Kentucky,...
Maombi ya Kiislamu ya kuswaliwa kwa jeneza la marehemu bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali yameanza hivi punde katika jimbo la Kentucky, Marekani.
Mohammed Ali
Ali alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 74.

Maelfu ya watu, wakiwemo Waislamu kutoka maeneo mengi duniani, wanahudhuria swala hiyo katika ukumbi wa Freedom Hall, mjini Louisville.
Mohammed Ali
Swala hiyo inapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga na Waislamu wengi duniani wanatumai kwamba itaashiria mchango mzuri kwa dini ya Kiislamu nchini Marekani.

Muhammad Ali alisilimu akiwa kijana. Alikuwa kwanza mwanachama wa madhehebu ya Nation of Islam, kundi lililotetea haki za watu weusi, lakini baadaye akakumbatia imani ya kawaida ya Kiislamu.

Mazishi yake yatafanyika Ijumaa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top