Ijumaa hii itakuwa tofauti kwa wateja wengi wa benki nchini. Ni kwasababu benki karibu zote kuanzia July 1, zitaanza kutumia sheria mpya ya fedha ya mwaka huu iliyopitishwa na bunge la 2016/17.

Kupitia tangazo lake kwa wateja, benki ya CRDB imedai kuwa ongezeko la asilimia 18 zitatozwa katika gharama za huduma ya benki kuanzia Ijumaa hii, July 1.
“Ongezeko hili (VAT) litakatwa kutoka katika akaunti na kama muamala hautapita kwenye akaunti, mteja atalipia kwa fedha taslimu, Kulingana na sheria hii, hakutakuwa na makato ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika riba,” imesema taarifa hiyo.
Benki ya NMB nayo imetoa taarifa hiyo kwa wateja wake.

Tags
HABARI ZA KITAIFA