DIAMOND AWAWEKA MASHABIKI NJIA PANDA BAADA YA KUTOA STATUS TATA

Msanii wa muziki, Diamond Platnumz ametoa kauli tata kuhusu uchawi na kuibua minong’ono mingi katika mitandao ya kijamii kuhusu wasanii kurogana.

Diamond Platnumz
Muimbaji huyo ambaye ana tuzo nyingi za kimataifa kuliko msanii yeyote nchini licha ya kukosa tuzo ya BET na kwenda kwa Black Coffee wa Afrika Kusini , alipost ujumbe wa ujio wa kazi yake mpya aliyowashirikisha wasanii wa kundi la P Square wa Nigeria huku akiwataka wenzake kutoa taarifa kwa waganga wao.

“Haya ongeeni vizuri na waganga wenu, baada ya siku nne naachia mashine nyingine,” aliandika Diamond kupitia twitter.

Kauli hiyo ya uchawi ambayo amekuwa akirudia rudia mara kadhaa katika mazungumzo yake, imewafanya mashabiki wa muziki kuamini kumbe wasanii wanatumia ndumba katika muziki wao.

Juni 5 mwaka huu, Diamond wakati akimtambulisha Rich Mavoko WCB, aliwataka waandishi wa habari kuacha kuchochea migogoro ya wasanii ili waganga na wao wapumzike.

“Watu wanapogombana tunaleta vita katika sanaa, familia, tuwapumzishe waganga na wao wanachoka, tunapeleka hela za bure,” alisema Diamond huku akicheka.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post