Leicester, ambao chini ya Meneja kutoka Italy Claudio Ranieri aliewahi kuiongoza Chelsea, sasa wamebakisha Mechi 2 na wana Pointi 77 na hawawezi tena kukamatwa na Tottenham wenye Pointi 70 na pia kubakisha Mechi 2.
Dakika ya 44, Pasi ya Eriksen ilimaliziwa na Son na kuandika Bao la Pili kwa Spurs.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 58, Gary Cahill aliipa Chelsea Bao la kwanza kufuatia Kona na yeye kumalizia vizuri.
Chelsea walisawazisha na Gemu kuwa 2-2 kwa Bao zuri la ushirikiano ambalo Eden Hazard alifunga kwa Shuti la juu la kupinda ambalo lilimshinda Kipa Loris.
Bila shaka, kuikata maini Spurs na kuwapa Ubingwa Leicester ndio lilikuwa lengo kuu la Chelsea na Mashabiki wao.
VIKOSI: Chelsea: Begovic, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Mikel, Matic, Willian, Fabregas, Pedro, Costa.
Akiba: Baba, Oscar, Hazard, Traore, Kenedy, Amelia, Loftus-Cheek.
Tottenham Hotspur: Lloris, Walker, Alderweireld, Vertonghen, Rose, Dier, Dembele, Lamela, Eriksen, Son, Kane.
Akiba: Mason, Vorm, N’Jie, Chadli, Wimmer, Carroll, Davies.
REFA: Mark Clattenburg
HIVI NDIVYO MASHABIKI WA LEICESTER CITY WALIVYOSHANGILIA UBINGWA WAO.
RATIBA LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi Mei 7
1445 Norwich v Man United
[Saa 11 Jioni]
Aston Villa v Newcastle
Bournemouth v West Brom
Crystal Palace v Stoke
Sunderland v Chelsea
West Ham v Swansea
1930 Leicester v Everton
Jumapili Mei 8
1530 Tottenham v Southampton
[Saa 12 Jioni]
Liverpool v Watford
Man City v Arsenal
Jumanne Mei 10
2145 West Ham v Man United
Jumatano Mei 11 [Saa 3 Dak 45 Usiku]
Norwich v Watford
Sunderland v Everton
2200 Liverpool v Chelsea
Jumapili Mei 15**Mechi za Mwisho za Ligi, zote kuanza Saa 11 Jioni
Arsenal v Aston Villa
Chelsea v Leicester
Everton v Norwich
Man United v Bournemouth
Newcastle v Tottenham
Southampton v Crystal Palace
Stoke v West Ham
Swansea v Man City
Watford v Sunderland
West Brom v Liverpool