NIJUZE NIJUZE Author
Title: YANGA SC SASA KUCHEZA KOMBE LA SHIRIKISHO BAADA YA KUTOLEWA NA AL AHLY, TAZAMA VIDEO YA MAGOLI HAPA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
WAKICHEZA Ugenini huko Borg El Arab Stadium Jijini Alexandria Nchini Misri, Yanga wamefungwa 2-1 na Vigogo wa Misri Al Ahly katika Mechi...
WAKICHEZA Ugenini huko Borg El Arab Stadium Jijini Alexandria Nchini Misri, Yanga wamefungwa 2-1 na Vigogo wa Misri Al Ahly katika Mechi ya Pili ya Raundi ya Pili ya CAF CHAMPIONZ LIGI na kutolewa nje ya Mashindano hayo.
Al Ahly
Yanga wametupwa nje kwa Jumla ya Mabao 3-2 baada ya Mechi ya Kwanza kwisha 1-1 Jijini Dar es Salaam.

Sasa Al Ahly wataingia Hatua ya Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI wakati Yanga wamechomekwa kwenye Droo ya Raundi ya Mchujo ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.

Kwenye Mechi ya Jana, Hadi Mapumziko Mechi hii ilikuwa 0-0.

Al Ahly walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 53 kupitia kwa Hossam Mohamed Ghaly na Yanga kusawazisha kupitia Donald Ngoma katika Dakika ya 67.

Bao la ushindi la Al Ahly lilifungwa Dakika ya 95 na Abdallah El Said.

Droo ya Raundi ya Mchujo ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho itafanyika huko Cairo hapo Aprili 21 na Mechi hizo kuchezwa kati ya Mei 6 na 8 kwa Mechi za Kwanza na za Pili ni kati ya Mei 17-18 na Washindi 8 kuingia Hatua ya Makundi.

Droo hii inajumuisha Timu 8 zilizosonga toka Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho na 8 zilizotolewa toka CAF CHAMPIONZ LIGI ambapo Timu toka Kombe la Shirikisho itapewa Mpinzani kutoka CAF CHAMPIONZ LIGI.

Timu zilizotoka Kombe la Shirikisho:
Angola - Sagrada Esperança
Egypt - Misr El-Makasa
Gabon - CF Mounana
Ghana - Medeama
Morocco - FUS Rabat
Morocco - Kawkab Marrakech
Tunisia - Espérance de Tunis
Tunisia - Stade Gabèsien

Kutoka CAF CHAMPIONZ LIGI:
Algeria - MO Béjaïa
Democratic Republic of the Congo - TP Mazembe
Libya - Al-Ahli Tripoli
Mali - Stade Malien
South Africa - Mamelodi Sundowns
Sudan - Al-Merrikh
Tanzania - Young Africans
Tunisia - Étoile du Sahel

VIKOSI: Al Ahly: Sherif Ekramy; Ahmed Fathi, Rami Rabia, Ahmed Hegazy, Sabry Rahil; Hossam Ashour, Hossam Ghaly, Abdallah El-Said, Momen Zakaria, Ramadan Sobhy; Amr Gamal


Yanga: Munishi, Abdul, Haroub, Joshua, Bossou, Kaseke, Msuva, Niyonzima, Kamusoko, Ngoma, Tambwe,
Akiba: Mustafa, Yondani, Issoufour, Nonga, Telela, Busungu, Twite

REFA: Mahamadou Keita [Mali]

HII HAPA VIDEO YA MAGOLI YOTE:

About Author

Advertisement

 
Top