WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI WALALAMIKIA KERO KUTOKA KWA WAZOAJI WA TAKATAKA WA MANISPAA

Wananchi wa Manispaa ya Lindi wameilalamikia Manispaa ya Lindi kuhusu utaratibu unaotumika katika ukusanyaji wa takataka.
Soko kuu lindi
Wamedai kuwa takataka zina kaa muda mrefu katika vizimba vya kukusanyia takataka hali inayoweza kupelekea kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na kadhalika.

Akiongea na Lindiyetu.com mwananchi aliye jitambulisha kwa jina la mama mtepa amelalamikia swala la kucheleweshwa kwa gari na ubaguzi katika swala la uzoaji taka hizo, hali inayo pelekea wanachi kubeba takataka wenyewe na kupeleka dampo.

Hamisi Mohamedi nae alitupia lawama zake kwa upande wa wazoaji hao kutokuwa na Ratiba maalumu ni lini takataka zinakusanywa, amesema hapo awali wali ambiwa kuwa gari itapita kukusanya takataka mara mbili kwa wiki lakini imekua kinyume kwani gari hazipiti kabisa hali inayo sababisha mrundikano wa takata majumbani.

WASIKILIZE WAKAZI HAO HAPA CHINI
Previous Post Next Post