Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo kwa klabu ya Simba kushuka uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kuikabili Mbeya City katika mchezo wao wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu soka Tanzani Bara msimu wa 2015/2016.

Simba ilishuka uwanja wa Taifa Dar Es Salaam ikiwa haina kumbukumbu ya kuwahi kuifunga Mbeya City katika uwanja huu zaidi ya sare na kupoteza, hivyo Simba kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Mbeya City, iakuwa imeweka rekodi ya kuifunga Mbeya City kwa mara ya kwanza uwanja wa Taifa Dar na mara ya pili kihistoria yake.
Magoli ya Simba yalifungwa kipindi cha pili, baada ya Awadh Juma kupiga shuti na kupanguliwa na golikipa wa Mbeya City Kalyesebula na Daniel Lyanga kupachika goli la kwanza kwa Simba dakika ya 75, Simba walifunga goli la pili dakika ya 90 kupitia kwa Ibrahim Ajib na kujihakikishia kukaa kilele mbele ya Yanga na Azam FC kwa tofauti ya point moja.

Tags
SPORTS NEWS