
Serikali ikiwa inapambana kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora za afya imekua kinyume katika Hospitali ya Mkoa wa Lindi kwani Hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa vitanda katika wodi ya akina mama wajawazito na watoto.
Kufatia changamoto hiyo inapelekea akina mama hao kulala watu wawili katika kitanda kimoja hali ambayo si mzuri kwa afya zao.
Changamoto nyingine ni uhaba wa watoa huduma katika wodi hiyo ya akina mama wajawazito.

Akiongea na Lindiyetu.com kaimu mganga mfawidhi Farida Ally amikiri uwepo wa changamoto hiyo pamoja na uhaba wa vyumba vya wagonjwa katika hospitalini hiyo.
*************************
TAZAMA GOLI LA MBWANA SAMATA DHIDI YA CHAD
Tags
HABARI ZA KITAIFA