NIJUZE NIJUZE Author
Title: PROFESA LIPUMBA, TUNDU LISSU WAKOSOA UTEUZI WA MUHONGO NA MWAKYEMBE, SABABU ZIKO HAPA WENYEWE WAELEZEA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Profesa Sospeter Muhongo Saa chache baada ya rais Magufuli kutangaza baraza lake la Mawaziri ambalo limekuwa baraza dogo kama alivyoa...
Profesa Sospeter Muhongo
Profesa Sospeter Muhongo

Saa chache baada ya rais Magufuli kutangaza baraza lake la Mawaziri ambalo limekuwa baraza dogo kama alivyoahidi, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu wamekosoa uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo na Dk. Harison Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe alikuwa waziri wa Uchukuzi katika serikali ya awamu ya nne na hivi sasa ameteuliwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria. Profesa Muhongo ambaye alijiuzulu kwa kashfa ya Escrow katika serikali ya awamu ya nne, amerudishwa katika wizara ya Nishati na Madini.

Profesa Lipumba amekosoa uteuzi wa profesa Muhongo kwa madai kuwa uteuzi wake umelitia doa baraza hilo.

“Kwa kitendo kama hiki, Rais Magufuli amejiwekea dosari kutokana na uteuzi huu. Maana yake ni kuwa katika kashfa ile Profesa Muhongo hakuwa na hatia,” Profesa Lipumba aliliambia gazeti la Mwananchi.

Profesa Lipumba aliongeza kuwa wananchi watapata ugumu kumuelewa Rais kutokana na ahadi zake kuwa atapambana na rushwa na ufisadi.

Naye Tundu Lissu aliliambia gazeti hilo kuwa uteuzi wa Dk. Harison Mwakyembe hakuwa sahihi kwa kuwa ndiye aliyekuwa waziri wa Uchukuzi na punde baada ya rais Magufuli kuingia ikulu, Mamlaka ya Bandari ikabainika kukumbwa na kashfa ya upotevu wa makontena.

“Juzi Rais Magufuli aliufumua uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kashfa, miongoni mwa waziri waliokuwa wakisimamia sekta hiyo ni Dk. Harrison Mwakyembe, eti leo amemrudhisha kundini?” Lissu ananukuliwa.

Lissu aliongeza kuwa Muhongo pia hakufaa kuwa miongoni mwa mawaziri kwa kuwa alifukuzwa na Bunge kutokana na sakata la Escrow.

Hata hivyo, Profesa Lipumba alimpongeza rais kwa kutekeleza ahadi yake ya kuunda baraza dogo kwa lengo la kubana matumizi.
Source: Mwananchi

About Author

Advertisement

 
Top