NIJUZE NIJUZE Author
Title: KASI YA MAGUFURI IMEIKUMBA HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI, MADIWANI WAIKATAA TAARIFA YA UTEKELEZAJI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Lindi. Ikiwa ni kikao chake cha kwanza tangu madiwani wa halmashauri ya manispaa tangu kuapishwa na kufanya uchaguzi wa ...
Lindiyetu Blogs News
Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Ikiwa ni kikao chake cha kwanza tangu madiwani wa halmashauri ya manispaa tangu kuapishwa na kufanya uchaguzi wa viongozi wa manispaa hiyo juzi.

Madiwani hao wameikataa taarifa ya utekelezaji wa shuguli za halmashauri hiyo katika kipindi cha kabla na baada ya zoezi la uchaguzi mkuu na wakati baraza lilipokuwa limevunjwa.

Madiwani hao walikataa taarifa hiyo iliyowasilishwa na mkurugenzi wa manispaa hiyo, Jomaaary Satura kwa madai kuwa ilikuwa haielewi na ilikuwa na kasoro nyingi.

Aliyeanza kuitilia mashaka na kuhoji ukweli wa taarifa hiyo alikuwa mbunge wa Lindi mjini, Hassan Kaunje. Mbunge huyo alisema taarifa hiyo haikuandaliwa vizuri na ilikuwa na mapungufu.

Ikiwamo baadhi ya miradi kuonesha imeanza kutekelezwa wakati bado haijaanza kutekelezwa. Kaunje alitolea mfano ufunguaji wa barabara mpya ya maeneo ya Kitumbikwela ambayo kwenye taarifa hiyo inaonesha imetekelezwa kwa asilimia 25.

Hata hivyo alipata mashaka kuwa kazi hiyo haijatekelezwa kwa kiwango hicho. Abeid Bakari, diwani wa kata ya Mtanda, alisema taarifa hiyo haikuwa imejitosheleza na kutoa maelezo ambayo yangewafanya wafuatilie ili kuhakikisha kama yaliyoelezwa yalikuwa yamefanyika.

Alisema taarifa hiyo inaonesha vikundi vya vijana na wanawake kupitia SACCOS vimepewa shilingi 42 milioni lakini haioneshi majina ya vikundi hivyo na mahali vilipo. Lakini pia kwenye taarifa hiyo inaonesha kuna vikundi vimepewa shilingi 38milioni, hatahivyo haijataja ni vikundi gani na vipowapi.
"Kwenye taarifa hii inaonesha kunanyumba ya mganga katika kijiji cha Kineng'ene, lakini kiasi cha fedha zilizotumika katika ujenzi huo hakionekani" hivyo naungana na wenzangu wanaosema taarifa hii haijakaa vizuri, ikaandaliwe upya iletwe kwenye kikao kijacho," alisema Abeid.

Diwani wa kata ya Matopeni, Selemani Namkoma, alisema kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kwenye taarifa hiyo, baraza halikuwa na sababu ya kuendelea kujadili. Badala yake irejeshwe kwa watendaji ikaandaliwe upya ili wawe na uwezo wa kufuatilia yatayoelezwa wajiridhishe kama yamefanyika au hayajafanyika.

Madiwani hao waliendelea kushikilia msimamo wa kutaka taarifa hiyo ikaandaliwe upya, ingawa mkurugenzi wa manispaa hiyo, Jomaary Satura kuwaeleza kuwa taarifa hiyo ni muhutasari tu.
"Siyo wajibu wangu kulazimisha, kwa kuwa watumiaji mnasema hamkubali, basi tutakwenda kurekebisha nakufanya mnavyotaka," alisema Satura.

Meya wa manispaa hiyo, Mohamed Liumbo licha ya kukubaliana na maagizo ya madiwani wenzake kuhusu suala hilo. wakati anafunga mkutano huo aliwaonya watendaji kuwa makini katika kutekeza majukumu yao. Alisema watendaji wa manispaa hiyo wasifanye kazi kwa mazoea, na watambue kuwa baraza hilo lina macho. Hivyo wajipange vizuri.

Naye mkuu wa wilaya ya Lindi, Yahya Nawanda aliwataka madiwani hao kuhamasisha wananchi wafanye kazi kwa juhudi na maarifa na wasimamie shuguli za maendeleo kikamilifu kwa madai kuwa wananchi hawaitaji porojo wala siasa bali maendeleo.

Kwa upande mwingine aliwaonya watendaji kuacha tabia ya kutoshugulikia na kuzitafutia ufumbuzi kero na matatizo wanayo ambiwa na wananchi.
"Hakuna sababu za kurundika matatizo, watendaji wa sekali za mitaa wanadanki(wanazurura) watendaji wa kata hawaeleki, malizeni na shugulikieni matatizo na kero za wananchi," alionya Nawanda.

About Author

Advertisement

 
Top