(PICHA HAIHUSIANI NA MADA HII)
Shirika la utangazaji la Ujererumani,DW limeripoti leo mchana kuwa idadi kubwa ya watu wameanza kuondoka mkoani Mtwara wakihofia hali ya usalama wakati wa uchaguzi.
Kwa mujibu wa Dw, watu wengi wanaoondoka ni wanawake na watoto, hali ambayo inaelezewa inatokana na vurugu za gesi za mwaka 2013, kuonekana kwa baadhi ya vifaa vya jeshi na wanajeshi wakiwa kwenye vifaru.
Soma walichokipost DW hapa chini....
Idadi ya watu wanaondoka katika mkoa wa Mtwara nchini Tanzania wakihofia hali ya usalama wakati wa uchaguzi imeongezeka na kuzidi kuongeza hofu katika jamii huku wengi wanaondoka katika mkoa huu ni wanawake na watoto, hali ambayo inaelezewa inatokana na kutokea kwa vurugu za gesi mwaka 2013 na kuonekana kwa baadhi ya vifaa vya jeshi na wanajeshi wakiwa kwenye vifaru.