TAZAMA VIDEO: LADY QUEEN AKIZUNGUMZIA UJIO WAKE NA SKENDO ZA KUFOJI

Queen wa ngoma ya 'Hakunaga' maarufu kwa jina la Lady Queen ambaye ni mwanadada mwenye umri wa miaka 23, 'Makelele na wewe' pia ni Track yake ambayo aliwahikufanya na Dullayo.
Lady Queen
Hapa ni wakati alipo fanikiwa kukutana na mwandishi wetu face to face ambapo mwandishi wetu alimtaka Lady Queen kuzungumzia Tasnia ya muziki wa hapa bongo kufuatia yeye ni mdau ambaye anategemea hapo baadaye aje kuishi maisha mazuri kupitia sanaa ya muziki. Baada ya msanii huyo ambaye anachipkia kwa kasi nzuri kupata fursa ya kufafanua muziki hiki hapa chini ndicho alicho zungumza.

LADY QUEEN: "Muziki wa Bongo fleva kiukweli umekuwa na ushindani mkubwa maana kila mmoja anatamani kufika mbali na kuwa juu ya mwenzie kwa kufanya vitu vizuri, so sasa hivi tunaangalia wakubwa zetu walifanya nini yaani ambao tayari muziki wao wameufikisha mbali mfano kama Vanessa, so nasisi tunaiga njia walizo tumia ili tuweze kufikisha na sisi muziki wetu panapotakiwa, kwa hatua hiyo naona tunaelekea pazuri kimuziki."

LADY QUEEN: "Naangalia kitu ambacho nikiimba kila mmoja atatamani kusikiliza watoto kwa wakubwa haijalishi ni wimbo wa mapenzi au laa! pia now nipokwenye mchakato wa kuboresha kucheza coz nafanya mazoezi ya kudance maana hata nikiwaga kwenye stage huwa natamani nicheze vizuri ili mashabiki wangu wa -Enjoy".

LADY QUEEN: "Kwenye muziki kiukweli ugumua ambao nauona ni kwenye kupata connection, maana hadi wadau wa muziki wakufahamu inahitajika juhudi ya kutosha, katika muziki wangu kitu ambacho naona kinamiss ni ushirikiano, maana baadhi ya mastaa wanatutenga sisi upcoming Artist unakuta mastaa kwa mastaa ndio wanakuwa na ushirikiano, so inakuwa ni ngumu kwetu kuyafikia malengo, mimi huwa najitahidi kuonesha ushirikiano kwa wasanii wote hasa kwa kuposta kazi zao ili basi hata namimi ninapo toa kazi zangu waweze kunisuport hata kwa kushare kazi ambayo nakuwa nimeitoa hiyo ni moja ya jitihada zangu."

LADY QUEEN: "Natamani sana kufikia level ya Vanessa Mdee na hata katika ndoto zangu ni kujakufanyanaye kazi, so kwa sasa najitahidi kutengeneza mazingira mazuri kwa kutoa kazi nzuri ili hata siku nikisema nimfuate kusiwe na ugumu wa yeye kukubali kufanya kazi na mimi I wish. Sitegemei kutoka kwa kukutumia skendo za kutengeneza maana nikitu ambacho nakishangaa sana coz unakuta msanii ni maarufu halafu anatengeneza skendo huko nikujishusha, nafuu sikendo ya kweli kuliko ya kufoji huo ni ushauri wangu kwa wasanii wanaopenda skendo."

LADY QUEEN: "Mwisho napenda kuwaambia mashabiki wangu kuwa nashukuru 'Hakunaga' wameipokea vizuri kinacho fuata ni zaidi ya 'Hakunaga' baada ya uchaguzi nitaachia Audio & Video ya wimbo wangu mpya ambao unaitwa 'Chunga Mzigo wako'. Stay tuned nawapenda sana."
Previous Post Next Post