ROMA AJISALIMISHA BASATA, KWA AJILI YA WIMBO HUU HAPA UNAOTOKA KESHO

Roma Mkatoliki ameamua kuchukua jukumu la kwenda Baraza La Sanaa Tanzania, BASATA kuwasikilizisha wimbo wake mpya anaotarajia kuuachia Jumapili siku ya uchaguzi Oct.25 ili waupe baraka kuepuka kufungiwa.
Roma Mkatoliki
Uamuzi huo umekuja kutokana na misukosuko aliyokutana nayo baada ya kutoa wimbo wake wa ‘Viva Roma Viva’ hivi karibuni, ambao BASATA waliufungia kutokana na madai kuwa hakuna ushahidi wa vitu vilivyoimbwa kwenye wimbo huo. .

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Roma alipost ujumbe huu siku ya Jumamosi Oct.24;

“Kesho Ndiyo Ile Tarehe Niliyowaahidi
Kuwa Nitaachia ‪
#‎KIBAO‬ Changu Kipya!!!!! /
Na Sasa Naelekea ‪#‎BASATA‬ Kuwasikilizisha Kabisa Kwanza!!! Wakitoa‪
#‎GO_A_HEAD‬ Tu Basi Kesho Alfajiri ‪#‎KINANUKA‬ / WAKIZINGUA NA MIMI NAWAZINGUA!!! /”
Previous Post Next Post