NIJUZE NIJUZE Author
Title: UPDATES:: MATOKEO RASMI YA MAJIMBO TOFAUTI TANZANIA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
UNGUJA-MAKUNDUCHI KUSINI UNGUJA-PAJE MKOA-LILUNDI  Hii ndio ripoti kuu ya NEC juu ya matokeo ya uchaguzi wa kura zilizo...
Lindiyetu Blog News

UNGUJA-MAKUNDUCHI
NEC
KUSINI UNGUJA-PAJENEC

MKOA-LILUNDI 
NEC


Hii ndio ripoti kuu ya NEC juu ya matokeo ya uchaguzi wa kura zilizopigwa jana katika uchaguzi mkuu Jimbo La Lulindi Mtwara. https://youtu.be/7xUpGeK5LHY





Hii ndio ripoti kuu ya NEC juu ya matokeo ya uchaguzi wa kura zilizopigwa jana katika uchaguzi mkuu Jimbo La Paje. https://youtu.be/gwVbujPU-bY




Tume ya Taifa Ya Uchaguzi Zanzibar imetangaza matokeo rasmi ya majimbo 2 ya ubunge na madiwani katika majimbo ya Fuoni Na Kiembesamaki. https://youtu.be/YKGnxP4NJ2E

UPDATES:: 4:36PM

Matokeo ya Uchaguzi yaliyonifikia hivi punde kutoka Jimbo la Nanyumbu mkoani Mtwara kwa nafasi ya ubunge yanasomeka kama ifuatavyo:
  1. DUA WILLIAM MKURUA(CCM) Kura 36175 sawa na 63%.
  2. MAJARIBU HASSAN LUPETO (CUF) Kura 13067 sawa na 23%.
  3. NYUCHI MANSA ALFRED (CHADEMA) kura 8182 sawa na asilimia 14%.
KWA UPANDE WA MADIWANI CCM IMEPATA VITI 15, CHADEMA KITI KIMOJA NA CUF KITI KIMOJA.

HUKU KATA YA LUMESULE ILIYOKUWA NGOME YA CUF IKIREJEA CCM.


MATOKEO YA SASA JIMBO LA NDANDA
  1. CESIL DAVID MWAMBE (CHADEMA) KURA 26247.
  2. MARIAM KASEMBE (CCM) KURA 26215.
  3. EDWARD MILLANZI (ACT WAZALENDO) KURA 923.
  4. ANGELUS THOMAS MILLANZI (NLD) KURA 447.
********************************
UPDATES:: 4:56PM

ESTER MATIKO (CHADEMA) ATANGAZWA RASMI KUWA MSHINDI WA KITI CHA UBUNGE TARIME MJINI
Ester Matiko
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Tarime Mjini, Bw. Mwanjombe amemtangaza rasmi Ester Matiko (Chadema) kuwa mshindi katika kinyang’anyiro cha ubunge wa jimbo hilo.

Matiko amekuwa mbunge wa kwanza kutangazwa rasmi huku akiweka histori kubwa katika wilaya ya Tarime mjini kuwa mwanamke wa kwanza kuwa mbunge katika wilaya hiyo inayosadikika kuwa na historia ya mfumo dume hususan katika ngazi ya familia.

Bi. Matiko amepata kura 20,017 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Kembaki Michael Mwita wa CCM aliyepata kura 14,025


*******************************************

UPDATES:: 5:26

MATOKEO YA SASA JIMBO LA LINDI MJINI
  1. SALUM KHALFAN BARWANY (CUF) KURA 18343.
  2. HASSANI SELEMAN KAUNJE  (CCM) KURA 20733.
Kwa matokeo Hayo Mshindi ni Hassani Seleman Kaunje wa Chama Cha Mapinduzi

Tutaendelea kuwajuza kila tunapopata matokeo.

About Author

Advertisement

 
Top