Muigizaji wa filamu nchini, Aunty Ezekiel amewakata Watanzania kuweka pembeni tofauti zao za kiitikadi na vyama baada ya uchaguzi kumalizika.
Akizungumza na Bongo5 jana, Aunty amesema amegundua watu wengi hawajui kuna maisha baada ya uchaguzi.
“Tunatakiwa kukubali kila kitu kinachofanyika katika uchaguzi kwa sababu wote tuna nia ya kulijenga taifa, kutetea haki ya mtanzania. Tunataka kuona watanzania wote tunakuwa katika hali nzuri. Sidhani kama mtu yupo upande mmoja ili kumuumiza mwenzie. Kila mtu yupo kuangalia analitengeneza vipi na kulijenga taifa letu ili watoto na ndugu zetu waje kuishi kwa amani,” ameongeza.
“Lakini nina imani watanzania kama watanzania hawajui kama kuna maisha baada ya uchaguzi. Kwa ushauri wangu ningependa watu wafahamu kuna maisha baada ya uchaguzi. Tusichukiane, tusiwekeane visasi, kwamba fulani alikuwa chama fulani! Kwahiyo ikitokea kama ni CHADEMA wameshinda tujue kama walikuwa wana haki tuwape nafasi ili wafanye kazi na kama ikitokea CCM ikashinda pia tuwape support ili kujenga taifa na maisha ya watanzania,” amesisitiza Aunty.
Uchaguzi mkuu wa Tanzania unatarajiwa kufanyika Jumapili October 25.