Unknown Unknown Author
Title: WAFANYA BIASHARA WA MADINI WAHAMASISHWA KUCHANGAMKIA SOKO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na.Ahmad Mmow,Liwale. Wafanyabiashara na wachimbaji wadogowadogo wa madini nchini wameshauriwa kuchangamkia soko kubwa la bidhaa hiyo lit...
Na.Ahmad Mmow,Liwale.
Wafanyabiashara na wachimbaji wadogowadogo wa madini nchini wameshauriwa kuchangamkia soko kubwa la bidhaa hiyo litakalofanyika jijini Arusha, mwezi Aprili mwakani.
Madini Liwale
Wito huo ulitolewa jana mjini Liwale mkoani Lindi na ofisa madini mkazi, wa wilaya za Liwale, Ruangwa na Nachingwea, Mayigi Likolobelo kwenye semina ya siku moja kwa wachimbaji wadogowadogo na viongozi wa baadhi serikali za vijiji, kata na tarafa za wilaya ya Liwale ambazo zimegunduliwa kuwa zinamadini.

Likolobelo alisema serikali kwa kutambua juhudi zinazofanywa na wafanyabiashara wa madini na wachimbaji wadogo wadogo, imekuwa ikijitahidi kutafuta masoko mazuri ili waweze kufaidika na juhudi zao. Ambapo imefanikiwa kupata soko zuri litakalofanyika mwakani mwezi Aprili, jijini Arusha. Hivyo amewaomba wachangamkie fursa hiyo adimu.

Alisema katika soko hilo zaidi ya nchi 20 zitashiriziki na wapeleka wafanyabishara wa madini ambao watakwenda kuuza madini. Kwa sababu bei za madini zitakuwa ni za kimataifa, kutokana kuwepo wanunuzi wakubwa kutoka katika mataifa mbalimbali duniani.

Ofisa huyo alisema hiyo haitakuwa mara ya kwanza, kwani soko la aina hiyo limewahi kufanyika katika jiji hilo na kwamba huo ni muondelezo wa juhudi za serikali za kuona wananchi wananufaika na kazi halali wanazozifanya, ikiwamo kwenye sekta ya madini.
"Kwahiyo nawaomba mjiandae ili muweze kushiriki na kutumia kikamilifu fursa hiyo," alisisitiza Likolobelo.

Pamoja na ushauri huo kwa wafanyabiashara na wachimbaji wadogowadogo. Ofisa huyo alitoa wito kwa viongozi wa ngazi zote katika Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kushirikiana na idara ya madini ili kuhakikisha shughuli zote zinazohusina na raslimali za madini zinafanyika kwa mujibu wa sheri ya mwaka, pamoja na kanuni zilizopo kwenye sheria hiyo.
"Hatua hii itasaidia kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima, na hivyo kukuza sekta ya madini na pia kuongeza mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa," aliongeza kusema.

Alisema. Mkuu wa wilaya ya Liwale, Ephraim Mmbaga, ambaye alikuwa ni mgeni rasmi wa semina hiyo. Aliwataka viongozi,watendaji wa serikali,wafanyabiashara na wachimbaji wadowadogo wa madini wilayani humo kuzingatia sheria na kanuni za madini ili kuondoa na kuepusha mgongano na maamuzi kwa vyombo vyombo vya serikali.
"Pia itumieni na kuwa na mawasiliano ya marakwara na ofisi ya madini ili mpate elimu itayowasaidieni kujua vizuri aina za madini na thamani yake,lakini pia mtasaidia kuepusha migogoro," alisema Mmbaga.

Mmoja wa wawashiriki hao, Rajabu Kwepu alisema miongoni mwa changamoto wanazopata ni pamoja na watafiti na wachimbaji wa madini ni kushindwa kutoa ushirikiano kwa serikali za vijiji na kutofuata sheria ndogondogo na taratibu lizowekwa na vijiji husika. Kwasababu leseni zao zimewahalalisha kuendesha shuguliza zao kwenye vijiji hivyo. Semina hiyo ya sikumoja ililenga kuwajengea uwezo wa kuzielewa kanuni na sheria ya madini ya mwaka 2010.

About Author

Advertisement

 
Top