Unknown Unknown Author
Title: MGOMBEA UBUNGE NACHINGWEA AAHIDI MAKUBWA, BOFYA HAPA KUJUA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na.Ahmad Mmow,Nachingwea. Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi octoba mwaka huu.Mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia Chama Ch...
Na.Ahmad Mmow,Nachingwea.
Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi octoba mwaka huu.Mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika jimbo la Nachingwea, Hassan Masala.

Lindiyetu Blog News
Amewahaidi wananchi wa jimbo hili iwapo atachuguliwa atahakikisha kila kituo cha afya kinapata gari ya kusafirisha wagojwa. Masala ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kibondo alitoa ahadi hiyo katika mikutano ya kampeni,kwa nyakati tofauti katika vijiji vya, Chiola, Chingunduli, Litula na Marambo.

Mgombea huyo anayechuana na wagombea wa vyama vingine vinne vya upinzani vya, ADC, ACT, CUF na CHADEMA. Alisema iwapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa mbunge, miongoni mwa viupaumbe atakavyoanza kuvifanyia kazi kwa kasi kubwa kuwa ni sekta ya afya ambayo inatanguliwa na sekta ya elimu. Ambapo katika sekta ya afya atahakikisha vituo vyote vilivyo katika jimbo hilo vinakuwa na magari ya kusafirishia wagonjwa.

Alisema miongoni mwa changamoto kubwa katika sekta hiyo ni usafiri na upungufu wa madawa katika vituo vya afya, hospitali na zahanati. Changamoto ambazo alihaidi kuzishugulikia haraka kwa madai kuwa afya ni mtaji wa awali wa binadamu katika kujiletea maendeleo.

Kuhusu sekta ya kilimo. Masala alihaidi kwa kushirikiana na viongozi wenzake kuandaa mazingira ya wakulima wenye mitaji, vikundi vya wajasiriamali na VICOBA vinakopeshwa matrekta ili waanze kulima kilimo cha kisasa.
"kuhusu sekta ya elimu ninauzoefu,kwani mimi kitaaluma ni mwalimu,natambua kuwa bila elimu hayo yote hayawezi kufanikiwa,hivyo nitasimamia ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika mazingira bora kwa walimu kuwa na nyumba mzuri na kuondoa tatizo la madawati," alisema Masala.

Sambamba na hayo, alihaidi pia kuharakisha uanzishwaji wa Redio ya halmashauri ya wilaya ya Nachingwea.

Alivitaja viumbele vingine kuwa ni mawasiliano, barabara, maji na Michezo. Huku akihaidi pia kusimamia kikamilifu ukasanyaji na usimamizi wa matumizi wa mapato wa ya halmashauri ya wilaya ya Nachingwea ili mapato hayo yawanufaishe wananchi wote badala ya wajanja wachache.

Wagombea wengine wa nafasi hiyo ni Moshi Matapula(ACT) Jordan Membe(CUF) Dkt Mahadh Mmoto(CHADEMA) na Haji Nanjase(ADC).

About Author

Advertisement

 
Top