Ukali zaidi wa maisha kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam unakuja kutokana na viwango vipya vya nauli za magari yaendayo haraka kuwa kati ya Sh. 500 hadi 900 kwa safari moja kwa mtu mzima. Aidha, nauli ya mwanafunzi itakuwa kati ya Sh. 250 na 450 kwa safari moja, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imetangaza jana.
Tangazo la Sumatra kwa vyombo vya habari jana lilieleza kuwa, mamlaka hiyo imepokea maombi ya nauli kutoka kwa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart) ambao utatoa huduma ya usafiri wa umma katika kipindi cha mpito.
Source: NIPASHE